Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali ya Tanzania yapongezwa utekelezaji miradi ya GPE LANES II na EP4R

Imewekwa tar.: November 22nd, 2024

Na Fred Kibano, Bunda, Mara

Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa kutekeleza miradi ya Elimu inayozingatia thamani halisi ya fedha, ubora wake na ushiriki wa jamii inapotekelezwa miradi hiyo.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Elimumsingi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwl. Suzan Nussu Nyarubamba akimwakilisha Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais TAMISEMI Atupele Mwambene leo tarehe 22 Novemba, 2024 wilayani Bunda mkoani Mara ambapo alisema wafadhiri hao wa GPE na EP4R wamekuja kujionea wenyewe kama utekelezaji wa miradi ya GPE LANES II, GPE TSP na EP4R imefanyika kama ilivyopangwa kwa ushirikiano na Serikali. 

“wageni wameridhika kwa kile walichokiona, kwanza thamani ya fedha kwenye miradi waliyotoa fedha, lakini pili ubora wa kazi zilizofanyika na tatu ushiriki wa Wadau mbalimbali katika shughuli zote za elimu kwani kila mahali tulipopita tumekuta Uongozi wa Kijiji, wajumbe wa Kamati ya Shule, walimu na baadhi ya wazazi wakitupokea na kuelezea utekelezaji wa miradi hiyo wakiwa kama sehemu ya timu inayotekeleza miradi” alisisitiza Mwl. Suzan Nussu Nyarubamba. 

Aidha, Mwl. Nyarubamba alisema baadhi ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan yametekelezwa kwa mfano Kampeni ya utoaji wa Lishe Bora kwa Watoto kwani kwenye shule walizopita na ugeni huo wamekuta watoto wanapatiwa chakula kulingana na vyakula vilivyopo kwenye maeneo yao hali inayopelekea mahudhurio kuwa mazuri kama ilivyo kwenye shule mpya ya msingi Ibwagalilo walipofanya ziara ambayo wanafunzi wake walikuwa wakienda umbali mrefu shule ya msingi Namalebe. 

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mheshimiwa Charlotta Ozaki Marcias alisema amefanya ziara hiyo na Wadau wa GPE, Wadau wengine na Serikali kwa kutembelea baadhi ya miradi shuleni kwenye mikoa ya Arusha na Mara ili kuona uhusiano wao na Serikali unadumishwa kwa kuangalia kazi zilizofanyika kwenye miradi ya elimu kama zimetekelezwa kwa mujibu wa malengo ya Serikali ya Tanzania.

Balozi Marcias pia ameridhika na jinsi elimu ilivyoimarishwa nchini kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, lakini pamoja na hayo amejionea mahitaji makubwa yaliyoongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi shuleni hususani baada ya Serikali ya Tanzania kuboresha Mfumo wa elimu na kuanza kutekeleza Sera ya Elimu Bila Ada.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Ibwagalilo Isack Sore ameishukuru Serikali na Wafadhiri wa GPE na EP4R waliofanya ziara shuleni kwake kwa kuwapatia fedha tangu mwaka 2019/2020 hadi mwaka 2023/2024 kwani walipokea shilingi 433,200,000 na kujenga madarasa 13, nyumba moja ya mwalimu, jengo la utawala, ofisi za walimu na matundu ya vyoo 42 ikiwa ni fedha kutoka GPE LANES II shilingi 46,600,00, EP4R shilingi 346,600,000 na Covid 19 shilingi 40,000,000.

Ziara hiyo ya siku nne imewahusisha Wafadhiri wa GPE na EP4R (Serikali za Sweden na Uingereza) na Serikali ya Tanzania ambayo imefanyika kwenye mikoani ya Arusha na Mara ili kujionea utekelezaji wa miradi hiyo ya Elimu chini ya GPE LANES II na Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ilivyotekelezwa.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.