Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Ruvuma, Songwe zatinga fainali UMISSETA 2019

Imewekwa tar.: June 19th, 2019

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Timu za mpira wa miguu za wavulana kutoka mikoa ya Ruvuma na Songwe ndizo zitakazocheza hatua ya fainali kumtafuta bingwa wa UMISSETA mwaka huu, mchezo unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Nangwanda  ijumaa tarehe 21 juni 2019.

Ruvuma ndiyo walikuwa wa kwanza kufuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Lindi kwa magoli 2-0. Magoli ya Ruvuma yakifungwa na Said Bakari dakika ya 29 na John Ching’uku alifunga goli la pili dakika ya 59.

Katika mchezo baina ya Mwanza na songwe ulilazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penati baada timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo na hatimaye Songwe kushinda kwa penati 4-3.

Shujaa  wa mchezo huo alikuwa ni golikipa wa Songwe Joseph Shibanda ambaye ndiye aliyewanyamazisha mashabiki wa Mwanza baada ya kudaka shuti kali la Felician Lucas wa Mwanza.

Penati nyingine kwa upande wa Songwe zilifungwa na Pascal Adriano, Joseph Shibanda, Michael kabuki pamoja na Justine Mwambungu huku penati ya Sekelo Kalinga ‘’kichuya mtoto’’ ikipanguliwa na golikipa wa mwanza.

Waliofanikiwa kufunga magoli kwa upande wa timu ya Mwanza ni  Nassoro Omary, Frank Faustino na Boniface Ernest huku waliokosa kwa upande wa Mwanza ni Mashinyali Maira, na Felician Lucas.

Kocha wa Songwe, Mwalimu PrayGod Lugenge amesema kuwa amefurahia timu yake kuingia fainali  kwani walijiandaa kwa muda mrefu baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu.

Alisema kuwa hashangazwi na timu yake kufika hatua hiyo kwani mwaka 2017 wakati wanashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza walifanikiwa kushinda mechi zao na hatimaye walitwaa kombe hilo ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano hayo.

Lugenge alisema kuwa timu yake pamoja na kucheza vizuri kwenye mchezo huo  ndani ya dakika 90 walilazimika kusubiri mchezo huo uamuliwe kwa penati baada ya timu yake kufanya mashambuzi mengi dhidi ya Mwanza.

Mwalimu huyo kutoka shule ya sekondari J.K Nyerere iliyopo Tunduma aliwataka wadau wa soka nchini hususan TFF kutafuta vipaji katika maeneo mengi nchini badala ya kung’ang’ania wachezaji wa Dar es salaam peke yake.

Amesema timu ya Songwe ina fursa ya kufanya vizuri kwani wachezaji wake wengi wanaundwa na timu nne za mkoa huo na hivyo wachezaji wake wengi wanafahamiana kwani wamecheza muda mrefu.

Aidha Kocha huyo wa Songwe ameisifu kamati ya kuratibu mashindano ya UMISSETA na  TAMISEMI kwa namna ilivyokuwa makini kuhakikisha kuwa mashindano ya mwaka huu hayatawaliwi na  mamluki.

Amesema mfumo wa kielektroniki uliotumiwa mwaka huu umerejesha msisimko uliokuwepo miaka ya nyuma ambapo wachezaji wanaoshiriki mashindano hayo ni wale wanaosoma katika shule za sekondari nchini.

Kwa upande wake nahodha wa Songwe Joseph Shibanda naye ameipongeza serikali kwa usimamizi thabiti wa michezo hiyo ambapo amesema kuwa kutokana na namna usimamizi ulivyokuwa mzuri utawezesha kupatikana kwa bingwa wa kweli na pia kuwezesha mikoa mingine kama Simiyu, Geita na Njombe kuwa na nafasi ya kushinda kombe hilo.

Wakati huo huo matokeo ya mpira wa kikapu yanaonyesha kuwa timu za kutoka mikoa ya Pwani na Shinyanga zitacheza hatua ya fainali kwa upande wa wavulana na timu za Mwanza na Dar es salaam zitakutana katika hatua hiyo kwa upande  wa wasichana.

Katika matokeo ya nusu fainali kwa kikapu wavulana Pwani iliwafunga Unguja kwa 66-32 na Tanga ilifungwa na Shinyanga kwa 47-55.

Kwa upande wa kikapu wasichana Mwanza iliwafunga Kilimanjaro 38-18 na Dar es salaam iliwafunga Morogoro kwa 38-17.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.