• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Rorya Wamkosha Dkt. Gwajima, mwenyewe Awapa Tano

Imewekwa tar.: November 4th, 2019

Halmashauri ya Wilaya ya Rorya imefanya vizuri katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unaondelea kujengwa hivi sasa, hali hiyo imepelekea Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika afya Dkt. Dorothy Gwajima, OR-TAMISEMI kutoa pongezi huku akiziagiza Halmashauri zingine kote nchini kuiga mfano wa Halmashauri hiyo. Siri ya mafanikio ya ujenzi huo uliofikia zaidi ya asilimia 80 umetokana na umoja, mshikamano na maelewano baina ya viongozi wa Halmashauri na Wilaya.

Akizungumza katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu, alisema hatua kubwa iliyofikiwa haina budi kupongezwa na kila mpenda maendeleo wa nchini, kwani yapo maeneo mengi ya nchi ambayo yalipata fedha za awamu ya kwanza shilingi bilioni 1.5 kama ilivyo Halmashauri ya Rorya, lakini mpaka hivi sasa wanabishana wapi Hospitali ijengwe huku wananchi wakiendelea kukosa huduma.

“Nikiri waziwazi kwakweli nyie mmekuwa wa mfano sana na hali hii ndio kurejesha fadhili kwa Rais wetu kipenzi cha watanzania Dkt. John Pombe Magufuli”, alisema Gwajima na kuongeza “ninatamani wengine wakaijua siri hii ya mafanikio, kwakuwa kuna Halmashauri huko sehemu zingine tulizopita ni vituko vitupu, pesa wamepelekewa toka Januari lakini hadi leo wanashindana wapi ijengwe Hospitali,” alishangazwa Dkt. Gwajima.

Kwa upande wao viongozi na Wataalam wa Halmashauri hiyo, walisema siri kubwa ni mshikamano na maelewano baina yao wenyewe lakini pia mawazo kutoka kwa wataalam.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Simoni Chacha, alisema, kikubwa walichokifanya mara baada yakupokea fedha walikaa kwa pamoja na kuweka mikakati ya namna ya ujenzi utakavyo endeshwa na kwakiasi kikubwa waliwashirikisha baadhi ya wataalam wastaafu.
“Sisi Mhe. Naibu Katibu Mkuu, hatukutaka kujifungia ndani wenyewe tuliwahusisha wataalam wastaafu, lakini sisi Kamati ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yote tulikubaliana lazima tuwasikilize wataalam kwa ushauri wao na sisi kama wasimamizi hatukupuuza ushauri wao” alisema Chacha.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya hiyo Charles Chacha, alisema mara kadhaa Mhandisi na Mganga Mkuu wa Wilaya na wataalam wenzao walipokutana na jambo likawatatiza, basi waliwaomba ushauri na walijadili kwa pamoja namna yakutatua tatizo.
“Mhe. Naibu Katibu Mkuu, kwakuwa hapakuwepo na muongozo wakuteua kamati baada ya mvutano niliamua kufanya maamuzi magumu ikiwapo hili lakuwashirikisha wataalam wastaafu akiwapo Afisa Ugavi wetu ambaye kila siku jukumu alilonalo ni jinsi gani anapokea vifaa na kuvitoa kwenye vitabu vyetu kwa utaratibu na kwakweli amekuwa msaada sana,” alisema Mkurugenzi.
Nao wataalama Wahandisi wanao simamia shughuli za ujenzi walisema, kufikia asilimia zaidi ya 85 ya ujenzi haikuwa kazi ndogo kwani kila mara wamekuwa wakifanya vikao eneo la kazi na kupitia kila kinachofanyika na wakifika mahali wakashindwa kuelewana wanakwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na   kwa aajili yakupata ushauri alisema Mhandisi wa Halmashauri hiyo.
Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, umefikia  asilimia zaidi ya 80 kwa majengo yote yaliyo elekezwa na serikali kujengwa, Majengo hayo ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje asilimia 88, jengo la Maabara asilimia 87, jengo la Mionzi asilimia 87, na jengo la uzazi asilimia 86. Majengo mengine ni jengo la ufuaji 87 pamoja na jengo la Utawala asilimia 84, huku wakitazamia kukamilisha asilimia zilizobakia ndani ya miezi miwili ijayo ili huduma kwa wananchi zianze kutolewa.  


Naibu Katibu Mkuu, yupo kwenye ziara yakukagua shughuli za Miradi ya Maendeleo hususan sekta ya afya, ambapo katika siku ya kwanza ametembelea Mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Rorya, Kituo cha Afya Otegi, Hospitali ya Mji wa Tarime , kituo cha Afya Magoma na Kituo cha Afya Nyamwaga ambacho   kilisajiliwa kama zahanati lakini kwa sasa kutokana uhitaji na ukarabati mkubwa unaoendelea, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ameomba kipewe hadhi ya Hospitali ya Wilaya.
MWISHO

Na Atley Kuni -MARA.

 

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.