Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Rais Dkt. Samia achangia shilingi milioni 50, kufanikisha ujenzi wa shule ya Msingi na umaliziaji wa majengo ya Zahanati inayomilikiwa na Bakwata Simiyu

Imewekwa tar.: October 13th, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha shilingi milioni 50, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya msingi na umaliziaji wa majengo ya zahanati inayomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania - BAKWATA mkoa wa Simiyu.

Harambee hiyo iliyoendeshwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa imewezesha kukusanywa kwa shilingi milioni 150 ikiwa ni ongezeko la shilingi milioni 20 zaidi ya shilingi milioni 130  iliyolengwa.

Harambee hiyo imefanyika usiku wa Oktoba 12, 2024, katika adhimisho la Maulid ya Mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2024, katika viwanja vya CCM wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza katika harambee hiyo Waziri Mchengerwa aliyepewa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika adhimisho hilo la siku takatifu ya kuzaliwa kwa mtume, amesisitiza umuhimu wa elimu dunia na elimu ya dini kwa jamii, akisema elimu ndiyo silaha na nuru ya kujikomboa dhidi ya majanga yote anayokabiliana nayo mwanadamu Pamoja na kupata utukufu.

Kulikazia hilo Waziri Mchengerwa ameiomba BAKWATA iweke miongozo itakayo wajenga waumini katika kusimamia kikamilifu Uzalendo, maadili na kuipenda dini, watu na nchi yao, kuanzia ngazi ya awali, na kusisitiza jamii na wadau mbalimbali wausishwe, watoa mafunzo waanishwe na wajengewe uelewa na uwezo wa maarifa na mbinu kwa maeneo ya vijijini na mjini.

Alikadhalika Ameshauri kufanyika kwa mapitio yatakayokuja na maboresho ya mfumo wa uendeshaji wa elimu ya dini ya kiislam kwa marika yote makubwa na madogo ili kuweka ulinganifu wa mafunzo sahihi ya dini ya kiislam nchini.

“Utaratibu huo uguse kwa kina na upana, kijiografia katika maeneo ya vijijini na mjini hadi yasiyofikika kwa urahisi, uandaliwe mpango mahususi wa uwekezaji kwenye eneo hilo  ili kuimarisha miundombinu  ya madrasa na mifumo yake ya uendeshaji kwa kuimarisha vyanzo vya ndani vya rasiliamli za aina zote kwa kuwahusisha waumini ili kuweka utengamano sawia kati ya maeneo ya vijijini na mijini” alisema Waziri Mchengerwa. 

Katika Harambee hiyo Waziri Mchengerwa amechangia kiasi cha shilingi milioni 10, huku Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akichangia shilingi milioni 50 na kufanya lengo lililokusudiwa awali la kukusanya shilingi million 130 kuvukwa hadi shilingi milioni 150.

Awali Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zuber miongoni mwa viongozi wakuu wa dini ya Kiislam walioshiriki katika Maulid hayo ameongoza dua ya kumshukuru na Kumwombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwataka waumini wote wa dini ya Kiislam kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura wa serikali za mitaa, katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea na zoezi hilo ili kuwapa sifa za kuwachagua viongozi wao katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.

Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.