Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Programu za Elimu ya Watu Wazima zitainua Elimu na Uchumi  wa Watanzania – Dkt. Emmanuel Shindika

Imewekwa tar.: October 11th, 2024

Na Fred Kibano Tabora

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Emmanuel Shindika amesema Programu za Elimu ya Watu Wazima zitasaidia  kuinua uchumi na elimu ya Mtanzania kutokana na uwekezaji na maboresho yaliyofanywa na Serikali na Wadau.

Dkt. Shindika akimwakilisha Mhe. Dkt. Dotto Biteko Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati aliyasema hayo wakati akifunga wiki ya Elimu ya Watu wazima iliyofanyika Kitaifa mkoani Tabora na kufikia kilele siku ya ijumaa tarehe 11 Oktoba, 2024 katika viwanja vya Chipukizi vilivyopo katika Manispaa ya Tabora.

“Serikali imefanikiwa kuwarejesha vijana waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa elimu ambapo vijana 12,000 wamenufaika na mafunzo ya muda mrefu na vijana zaidi ya 30,000 wakinufaika na mafunzo ya muda mfupi yanayolenga kuwandaa kuwa na ujuzi wa kiufundi na biashara ambao unawasaidia kuanzisha miradi ya kiuchumi inayochangia kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa hii inasaidia kuwapa fursa wale waliokatishwa masomo yao au waliokosa nafasi ya kuendelea na elimu kupitia mfumo rasmi, hivyo kuwapa nafasi ya kujikomboa kielimu na kiuchumi” alisema Dkt. Shindika.

Alisema Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kukishirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wanatekeleza Mradi wa Elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi ambapo katika mwaka wa masomo 2024 wanafunzi wapatao 18,886 wameweza kudahiliwa na elimu hii inatolewa kupitia vituo vya shule huria (Open Schools) vipatavyo 763. Pia Programu za mafunzo ya ujasiriamali, ufundi na teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) zimewawezesha vijana na watu wazima waliokuwa nje ya Mfumo Rasmi wa elimu kujipatia ujuzi wa kiteknolojia unaowezesha kuongeza uzalishaji katika sekta mbalimbali za viwanda, kilimo na biashara.

Kwa upande wake Abdul M. Maulid, Kaimu Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alisema maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya na  yana umuhimu wa kuhakikisha elimu inawafikia watu wote na ni nyenzo muhimu ya kuwawezesha watu wazima kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi hasa wakati huu ambapo yanatokea mabadiliko makubwa ya Kisayansi na Kiteknolojia Duniani.

Akitoa salamu za awali Upendo Rweyemayu Afisa Elimu Mkoa wa Tabora alitoa rai kwa wanatabora kuhakikisha wanawaandikisha watoto wao kuingia darasa la kwanza mwaka 2025 pamoja na kuwahimiza wanafunzi watoro sawa na asilimia 40 ambao hawafiki shuleni ili kupunguza tatizo la watu wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu miaka ya mbele.

Naye Ayoub Kafyulilo Mratibu wa masuala ya Elimu UNICEF Tanzania alisema kwa Tanzania wanatekeleza Mradi wa Elimisha Mtoto unaolenga kuhakikisha Watoto wote waliokosa elimu katika mfumo rasmi wanapatiwa elimu, na Mradi wa Elimisha Mtoto wa kike kuwawezesha watoto wa kike kufikia ndoto zao.

Juma la Elimu ya Watu Wazima limefikia kilelel tarehe 11 Oktoba, 2024 na wananchi wa Tabora walijitokeza kujifunza kuhusu Programu zake na baadhi ya Wadau wanaofadhili afua mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi walihudhuria ambao ni UNICEF, UNESCO, CARE International, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na DVV International huku kauli mbiu ya mwaka 2024 ni ‘Ujumuishi katika Elimu bila Ukomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu, Amani na Maendeleo’

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.