Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

MSIKWAMISHE MIRADI YA SEQUIP - Silinde

Imewekwa tar.: June 29th, 2022

Na Fred Kibano

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Davidi Silinde, amesema kwa uzembe wowote utakaofanyika kwa ajili ya kukwamisha Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naibu Waziri Silinde ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma hivi leo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa wa mazingira kuhusu masuala ya usalama wa Mazingira na Jamii katika kutekeleza mradi wa SEQUIP.

Amesema kwa mtendaji ambaye atajaribu kukwamisha Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) hataweza kuvumiliwa na kabla hajachukuliwa hatua ni lazima ajitafakari.

Silinde amesema kuwa Serikali kupitia mradi wa kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika mwaka wa fedha 2020/22 Serikali imetumia fedha kwenda kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kiasi cha shilingi billion 139.57 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za sekondari.

Amesema kuwa Serikali imetumia fedha kwenye mamlaka za serikali za mitaa takribani sh.bilioni 139.57 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za sekondari 243 zikiwemo shule 10 za sekondari za bweni za Mikoa kwa ajili ya wasichana na shule 232 za sekondari za kata katika kata ambazo hazina shule na kata zenye wanafunzi wengi ukilinganisha na miundombinu ya shule iliyopo.

Silinde amesema kuwa utekelezaji wa Mradi huo ni kwa ajili ya kutatua changamoto ya ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa katika shule za sekondari nchini kutokana na utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo ambapo idadi ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari imeongezeka.

"Mradi huu wa SEQUIP umekuja wakati ambapo kumekuwa na mwitikio mkubwa katika uandikishaji wa wanafunzi na hivyo kusababisha ongezeko la Mahitaji ya miundombinu kwa ajili ya kupokea wanafunzi wanaijiunga na Elimu ya Sekondari" alieleza Silinde.

Amesema kwa mfano katika mwaka 2021 wanafunzi wa elimu ya Awali, Msingi na Kidato cha kwanza walikuwa 3,469,275 ambapo kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 472,969 walioandikishwa mwaka 2022 na kufikia wanafunzi 3,942,244 sawa na ongezeko la asilimia 14”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu TAMISEMI, Ephraim Simbeye akiongea kwa niaba ya Naibu Karibu Mkuu TAMISEMI Dkt.Charles Msonde amesema kuwa mradi wa SEQUIP  unatarajiwa kutekelezwa katika eneo la Elimu ya Sekondari kidato cha kwanza hadi cha sita kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020/2021hadi 2024/2025.

Alisema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa utaratibu wa Lipa Kulingana na Matokeo ambapo motisha ya fedha hutolewa kwa Serikali baada ya kufikia matokeo yaliyokubalika kwa kuzingatia viashiria vya mradi.

Aidha Simbeye alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuleta mafanikio na maboresho makubwa katika eneo la Elimu ya sekondari.

Amesema utawasaidia wanafunzi wapatao milioni 6.5 kumaliza elimu ya sekondari na stadi za maisha ambapo kati yao wanafunzi wasichana ni milioni 3.2 wakiwemo wasichana waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali.

Naye Julius Achiula Mtaalam wa Mazingira mkoa wa Arusha na Mratibu wa SEQUIP Kanda ya Kaskazini ikihusisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga ametoa ombi la kupatiwa vitendea kazi ili kujengewa uwezo pamoja na kuwa wamejengewa uwezo na hayo yakiwa mafunzo ya awamu ya tatu.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.