Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mradi Hospitali ya Wilaya Bunda Hoi, Serikali yawapa siku 30 Tu

Imewekwa tar.: November 5th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anaye shughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa siku thelathini kuanzia Oktoba 05, 2019 kwa Halmashauri ya Wilaya Bunda mkoani Mara, iwe imekamilisha miradi yake yote yenye utata na ianze kutoa huduma kwa wananchi ifikapo tarehe 05 Desemba, 2019. Dkt. Gwajima ameagiza pia jopo la wataalam kutoka OR-TAMISEMI kwenda wilayani humo kufanya ukaguzi maalum kwa miradi yote yenye sintofahamu na kutolea taarifa ya kina.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo hivi leo wakati wa ziara yake inayoendelea kwenye mikoa ya kanda ya ziwa ambapo alionekana kutoridhishwa na mwenendo wa miradi ya Halmashauri  hiyo husuani  ni ule wa Hospitali ya Wilaya ambao ulipokea fedha kutoka Serikalini kiasi cha bilioni 1.5 kutoka mwezi Januari, 2019, lakini ujenzi wake ukachelewa kuanza hadi ilipofika mwezi Mei, 2019 huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni  malumbano baina ya viongozi wa eneo hilo.  

“Kwakweli mimi ambaye nimepewa dhamana yakusimamia eneo hili kwa mwendo huu sijaridhika  kabisa., siku ya jana nilikuwa Halmashauri ya Rorya, Umoja, ushirikiano na kutenda kazi kwa mshikamano nilio uona pale siuoni kabisa ndani ya Halmashauri hii ya Bunda” alisema Dkt. Gwajima na kuongeza kwamba, “ninataka ndani ya siku 30 yaani mwezi mmoja kuanzia sasa Mkurugenzi, Miradi yote inayo lalamikiwa iwe imekamilika na taarifa tuipate TAMISEMI” aliagiza Dkr. Gwajima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kusaja Amos, ilionesha, katika mwaka wa fedha wa 2018/19, Halmashauri ilipokea kiasi cha bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hata hivyo kutokana na malumbano baina ya viongozi hao, shughuli rasmi za ujenzi zikaanza  Mwezi Mei, 2019 na ilipofika tarehe 31 Juni,2019 fedha zote ambazo zilikuwa hazijaingia katika mpango wa manunuzi zilirejeshwa hazina kama sheria za fedha zinavyo elekeza.

Pamoja na Mkurugenzi kujitetea mbele ya Naibu Katibu Mkuu kuwa, ujenzi huo umefikia asilimia 70 ya ujenzi wote hali ni tofauti na uhalisia kwani hadi siku ya ziara hiyo baadhi ya Majengo yalikuwa ndio kwanza yanamwagiwa zege ili yaanze kunyanyuliwa.

“Mkurugenzi ukisema jengo limefikia asilimia 50, tutegemee kuona majengo yote yaliyoelekezwa yawe yamefunikwa na mmeanza umaliziaji, sasa wewe hapa ndio kwanza majengo takrinan manne ndio yameanza kupigwa paa na kuezekwa na jengo lingine ndio kwanza wanamwaga zege wewe unasema asilimia 70 huku sikuudanganya umma wa watanzania?” Alihoji Dkt. Gwajima.

Kufuatia kulalamikiwa kwa miradi mingi ya Halmashauri hiyo, ikiwapo ule wa ujenzi wa Ofisi ya Mbunge, Zahanati ya Namababe pamoja na  kituo cha Afya Mugeta kilichopelekewa fedha kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu lakini hadi siku ya Ziara ya Naibu Katibu Mkuu kulikuwa na kasoro nyingi za kitaalamu ili mlazimu Naibu kutoa msimamo wa serikali.

Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu akiwa katika ziara hiyo, amewaelekeza wakurugenzi  kote nchini kufanya sensa ya watumishi waliojiendeleza  kielemu na sasa wapo tayari kufanyiwa recategorization lakini bado wanasomeka kwenye miundo ya zamani ilihali kimajukumu wameongezewa mzigo wafanye utaratibu huo haraka ikiwapo kuwatengea nafasi.

“Nitumie fursa hii nikiwa hapa katika kituo cha Nyasho mjini Musoma, kupeleka salaamu zangu kwa Wakurugenzi na Maafisa Utumishi, wapitie na kufanya sensa kubaini watumishi wanaohitaji kubadilishiwa vyeo vya muundo, lakini kwa hila tu za Afisa  mtumishi, mtumishi amekaa zaidi ya miaka saba katika cheo cha zamani na hajabadilishiwa kazi lakini anapewa majukumu ya kazi mpya bila maslahi yake kuboreshwa hii haikubaliki.” alikemea Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima alikuwepo katika ziara ya ufatiliaji utendaji kazi na hali ya miundombinu ya Afya ambapo katika siku yake ya pili alitembelea na kukagua vituo cha Afya Nyasho na Makoko vyote vya Mji Musoma, Hospitali ya Wilaya ya Musoma vijijini inayoendelea kujengwa, Hospitali ya Wilaya Halmashauri ya Bunda ambayo imepewa siku 30 iwe imekamilika  sambamba na Zahanati ya Mugeta zote za Bunda Vijijini.

Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI, Bunda

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.