Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

MPANGO WA UWEKEZAJI AFYA YA MAMA NA MTOTO WAZINDULIWA ZANZIBAR

Imewekwa tar.: August 23rd, 2023



Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman amezindua Mpango wa Uwekezaji wa Afya ya Mama na Mtoto Tanzania wa miaka mitano (Tanzania Martenal & Child Health Investment Program) wenye lengo la kuimarisha afya ya Mama na mtoto nchini  unaofadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Global Financing Facility. 


Akizundua Mpango huo leo Agosti 23,2023 Zanzibar .Mhe Othman amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Dkt. Samia Suluhu Hassan  na Rais wa  Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi  kwa kuendelea kutoa kipaombele katika sekta ya afya  na  kuwezesha uzinduzi wa mpango  wa uwekezaji  katika afya ya mama na mtoto unaolenga kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto katika ngazi zote Tanzania Bara na Zanzibar.


Amesema Mpango huo utatekelezwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya Tanzania Bara,  Wizara ya Afya Zanzibar pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo uwekezaji wake utagharimu dola za Marekani milioni  275 na kati ya hizo dola za Marekani 250 ni mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Dunia na  dola za Marekani milioni 25  kutoka Global financing facility.


Mhe. Othman amesema  kuwa, kwa upande wa Tanzania Bara Mpango huu utatekeleza afua muhimu ikiwemo kuajiri watumishi 1, 000 wa kada mbalimbali za afya, kufanya ukarabati wa vituo 159 vya kutolea huduma za afya na ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto. 

Sanjari na hilo Mhe. Othman amesema mpango utaimarisha mfumo wa magonjwa ya dharura na rufaa kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga pamoja na kuimarisha menejimenti na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya na  kwa upande wa Zanzibar mpango  utaimarisha utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto pamoja na  kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi. 


Naye, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Festo Dugange amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI  itasimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji wa Afya ya Mama na Mtoto (Tanzania Maternal & Child Health Investment Program)  kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa  ili kufikia  malengo yaliyokusudiwa  na Serikali.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya Tanzania Bara Mhe. Godwin Mollel amesema Serikali itasimamia kikamilifu fedha zitakazotolewa ili kufikia lengo la kuboresha huduma za afya kwa jamii.

Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.