Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mhe. Magufuli awashukuru wadau wa maendeleo wa mfuko wa pamoja wa afya

Imewekwa tar.: April 9th, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Afya Nchini kwa kujitoa kwa hali na mali katika kusaidia kufanikisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya Afya nchini

Ameyasema hayo leo wakati akifungua kituo cha afya cha Madaba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba , Mkoani Ruvuma,  moja ya vito 352 vilivyojengwa kupitia wadau wa maendeleo wa  sekta ya afya  nchini.

Mhe. Magufuli amewashukuru wadau hao kwa mchango mkubwa katika    ufanikisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya nchini jambo ambalo limeleta mabadiliko na kupunguza changamoto zilizokuwa zinaikabili  sekta ya afya nchini.

Mhe. Magufuli amefafanua kuwa sekta ya afya ni muhimu katika maendeleo ya taifa kwani watu wasio na afya njema ni ghrama kubwa kwa taifa na hudumaza maendeleo ya nchi, hivyo serikali imeamua kuwekeza katika Sekta ya afya ili kuwa na wananchi wenye afya bora ili kufikia uchumi wa kati..

“Ripoti ya shirika la afya duniani inaonyesha kuwa nguvu kazi iliyopotea kwa sababu ya magonjwa barani Afrika  ni sawa na saa milioni  630 na inaonyesha kuwa endapo nchi za Afrika  zitashindwa kuwekeza vizuri kwenye masuala ya afya zitapoteza wastani wa dola za kimerikani trioni 2.24 kwa mwaka hiki ni kiasi kikubwa sana  cha upotevu wa muda hivyo  kulitambua hilo  Serikali iliamua  kuwekeza kikamilifu katika sekta ya afya”Amesema Mhe. Magufuli.

Ameendelea kusema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya afya ili kuweza kuwasaidia wananchi wa hali ya chini ambao wanachangamoto kubwa katika kupata huduma karibu na maeneo yao.

Mhe. Magufuli amesema Serikali kwa sasa imebadilisha utaratibu wa kuhakikisha fedha zote za ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya nchini zinapelekwa moja kwa moja kwenye vituo husika ili ziweze kutumika kwa malengo yalioyopangwa na kuleta mabadiliko katika vituo hivyo.

Aidha amewapongeza wananchi na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuhakikisha wanasimamia kwa umakini mkubwa ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya, jambo ambalo limesaidia vituo hivyo kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa jamii.

Wakati huohuo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Senkamba Kandege amewashukuru wadau  wa Mfuko wa afya wa pamoja (Basket Fund), wananchi na watumishi wa Serikali za Mitaa kwa kujitoa kwao katika  kufanikisha utekelezai  wa mikakati wa maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini.

Mhe. Kandege amesema kituo cha Afya cha Madaba ni miongoni mwa vituo vya kutolea Huduma za Afya 352 ambavyo vimekarabatiwa na kujengwa kupitia mpango wa maboresho wa afya msingi nchini

Amefafanua kuwa Kituo cha Madaba kimejengwa kwa gharama shilingi milioni 665 ambapo shilingi milioni 220 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba, milioni 445 zilitumika  katika ujenzi wa kituo hicho.

Ameleeza mchanganuo wa fedha hizo na kusema kuwa  shilingi milioni 400 zimetoka katika mfuko wa afya wa pamoja,  shilingi milioni 7.2  ni nguvu za wananchi wa Madaba  na  shilingi milioni 38.3  ni kutoka makusanyo ya  ndani ya Halmashauri  ya Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma.

Aidha Mhe. Kandege amesema kuwa OR-TAMISEMI imeweka mikakati ya kuboresha huduma za afya  kuanzia ngazi ya msingi kwa kukarabati miundombinu  katika vituo vya afya 535 nchini ifikapo mwaka 2020 ambapo mpaka sasa  vituo 304 vimekamilika lengo ni kuhakikisha maboma  1885 yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi yanakamilika.

Na. Angela Msimbira  RUVUMA



Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.