Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mfumo wa uhasibu kuongeza uwazi na uwajibikaji katika halmashauri

Imewekwa tar.: June 5th, 2018

Na Mathew Kwembe, Iringa

Serikali imesema kuwa maboresho iliyoyafanya kwa kushirikiana na Mradi wa PS3 ya kuwa na mfumo mmoja wa uhasibu ujulikanao kama Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma, (epicor) tolea la 10.2  ni  hatua kubwa katika utekelezaji wa dhana nzima ya uwazi, uwajibikaji na utawala bora katika usimamizi wa Fedha za umma na kuboresha huduma kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Iringa na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Baltazar Kibola, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Epicor toleo la 10.2 kwa Wahasibu na WawekaHazina kutoka Mikoa ya Morogoro, Iringa  na Halmashauri za Jiji la Tanga, Muheza na Korogwe.

Bwana Kibola alifafanua kuwa kutokana na maboresho yaliyofanyika ya kuwa na mfumo mmoja wa usimamizi wa fedha za umma sasa itakuwa rahisi kwa viongozi wa serikali kuweza kufuatilia taarifa mbalimbali za serikali katika halmashauri zote 185.

“Katika mfumo huu wa usimamizi wa fedha haitakuwa rahisi mtu kubadilisha taarifa, na hii itaongeza uwazi, na uwajibikaji, na pia itachochea kuboreshwa kwa huduma wazipatazo wananchi,” alieleza.

Bwana Kibola aliongeza kuwa mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma, (epicor) tolea la 10.2 utawezesha mifumo yote ya msingi ya usimamizi wa fedha katika sekta za umma kuwasiliana na kushirikishana katika suala la utoaji wa taarifa.

“Kupitia mafunzo ya Epicor toleo la 10.2 washiriki watajengewa uwezo kujua namna mifumo ya PlanRep (Mipango na Bajeti), FFARS (Usimamizi wa Fedha zinazopelekwa na Serikali moja kwa moja kwenye vituo) na LGRCIS (Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya Halmashauri) zitakavyobadilishana taarifa kupitia mfumo wezeshi wa Muungano Gateway,” alieleza.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo msaidizi, maboresho yaliyofikiwa kwenye mfumo wa Epicor 10.2 yatasaidia katika suala zima la utoaji wa taarifa hasa kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma pamoja na kuunganisha taarifa hizo kwenye Hesabu za Halmashauri, pia utatoa taarifa za utekelezaji za mipango na bajeti kwa kuzingatia matumizi ya fedha yaliyofanyika.

Naye Mweka Hazina kutoka jiji la Tanga bwana Cornery Sima alieleza kuwa mfumo wa Epicor toleo la 10.2 utasaidia kutatua changamoto za kutoonana kwa mifumo hiyo, ambapo sasa mifumo minne ya uhasibu imeunganishwa na kuwa kitu kimoja.

Aliongeza kuwa mbali na kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwani sasa taarifa zitakuwa zikionekana popote kwa kuwa mfumo wake utakuwa ni mmoja.

Pia alisifu kuwepo kwa mifumo ya kihasibu kwani itapunguza matumizi ya kutumia makaratasi, ambapo tofauti na kuandika hundi kwa njia ya mkono, mfumo huu wa malipo umeunganishwa moja kwa moja na benki kuu.

Mapema mgeni rasmi kwenye mafunzo hayo Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bibi Wamoja Ayubu alisema kuwa lengo la kuwajengea uwezo ili muweze kusimamia mapato na matumizi ya Fedha za Umma kwenye Halmashauri na pia kuwapatia uelewa wa mabadiliko ya msingi yaliyofanyika bila kukwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aliongeza kuwa wao kama Makatibu Tawala wa Mikoa, ambao ni viongozi wa Mikoa watahakikisha matumizi sahihi ya mifumo yanakuwepo ikiwemo matumizi ya taarifa katika kufanya maamuzi kuanzia ngazi za vituo vya kutoa huduma mpaka ngazi ya Mkoa.

Mafunzo hayo ya Mfumo wa Epicor toleo la 10.2 kwa Waweka Hazina, Wahasibu, Maafisa Manunuzi, Maafisa TEHAMA pamoja na Maafisa Usimamizi wa Fedha wa Mikoa yataendeshwa na wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), wakishirikiana na wataalam kutoka mradi wa PS3.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.