Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

MCHENGERWA ATOA MIL.40/- KUSAIDIA WANANCHI WA RUFIJI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Imewekwa tar.: April 3rd, 2024

Na. Projestus Binamungu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh.milioni 40 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu kwa zaidi ya wakazi 1,000 wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji ambao mali, mashamba na makazi yao yameathiriwa na mafuriko ya maji, yaliyofunguliwa kutoka bwawa la uzalishaji umeme la Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na wakazi hao mara baada ya kufanya ziara ya kukagua athari ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, Waziri Mchengerwa amesema analazimika kutoa kiasi hicho cha pesa ili kuwatia moyo wakazi hao kurejea shambani kulima upya baada ya mazao yao kusombwa na mafuriko hayo.

“Hili ni janga letu sote mimi na nyinyi, tuliamini kwamba ujenzi wa JNHPP utakuwa mkombozi wa mafuriko ambayo yamekuwa yanatukumba mara kwa mara lakini kwa bahati mbaya bado imejitokeza, tuendelee kuwa na Imani kwamba mradi ukikamilika uwenda changamoto hii ikawa imetatuliwa” alisema Waziri Mchengerwa.

Aliongeza kuwa “ Ninafahamu fika namna wakazi wa Rufiji mlivyokuwa mmelima kwelikweli mwaka huu, ninaomba turejee shambani tulime tena vilevile kwa kiwango kikubwa, mimi ninamkabidhi Mkuu wa wilaya shilingi milioni 40 kwa kuanzia kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu ili turejee shambani tupande tena tusije kufa kwa njaa”

Alikadhalika Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa taasisi na mashirika ya misaada ya kibinadamu Pamoja na wasamalia wema kuguswa na hali ya Warufiji kwa kuwashika mkono kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki ambacho serikali ya wilaya inaendelea na ufuatiliaji na tathimini ya athari za mafuriko hayo kwa ujumla.

“Ukweli niseme kiasi hiki cha milioni 40 nilikuwa nimekidunduliza kutoka kwenye mshahara wangu kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa na futari ya Pamoja katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kama tunavyofanya kila mwaka, lakini kwa hali hii ya mafuriko niseme tu kwamba futari si kitu nalazimika kutoa kiasi hiki kwa ajili ya ununuzi wa mbegu na nitaenda kuwaomba marafiki zangu wanichangie angalau tufikishe milioni 100 kwa ajili ya kusaidia warufiji walioathirika na mafuriko haya” Aliongea Waziri Mchengerwa.

Halima Mbwana mkazi wa Kijiji cha Chumbi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa mafuriko hayo amedai kuwa hali inazidi kuwa mbaya kuanzia chakula, marazi na makazi na hivyo wanatamani kupata wasamalia wa kuwashika mkono.

“Tumesalia watupu, mazao shambani yamesombwa na maji na hata vyakula vya ziada tulivyokuwanavyo vimesombwa pia, nyumba nazo zimesombwa na maji sasa hatuna pa kuishi wala hatuna chakula, tunaomba tusaidiwe maana hali zetu ni mbya kwakweli” alisema Mbwana.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele tathimini ya awali imebaini kuharibiwa kwa nyumba 58, na jumla ya wakazi 951 waliokuwa wakiishi kwenye maeneo ya vitongoji vya Kanga,Kiegele, Kilindi na Nyandote katika kata ya Chumbi wameondolewa katika maeneo yao nakuhamishiwa sehemu salama, huku zaidi ya hekta elfu 28,374.74 za mazao ya kilimo na bishara kama vile mahindi, Mpunga, Ufuta nan dizi zikiathiriwa na mafuriko hayo.

Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.