Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

MAAFISA ELISHE TOENI ELIMU YA LISHE KWA JAMII

Imewekwa tar.: July 17th, 2023

 OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dkt. Charles Mahera amewataka maafisa lishe nchini kutoa elimu kwa jamii ili kuepuka udumavu kwa watoto. 

Dkt. Mahera ametoa wito huo leo Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi inayofanywa kwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dtk.Grace Magembe kukagua utoaji na ubora wa huduma kuanzia ngazi ya msingi hadi rufaa, ambapo wamekagua hali ya utoaji Huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  Iringa na Hospitali ya Halmashauri ya Iringa Frelimo.

Dkt. Mahera amesisitiza maafisa hao kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya udumavu kwa watoto hasa wenye umri chini ya miaka nane na namna ya kuwatangenezea chakula chenye lishe. 

“Tujitahidi kutoa elimu kwenye jamii zetu kwani madhara ya udumavu katika umri mdogo unapelekea watoto kutoelewa vizuri darasani pindi wanaposoma na kuleta madhara ya kudumu pale wanapofikisha umri mkubwa”, ameeleza Dkt. Mahera. 

Hata hivyo Dkt. Mahera amewataka maafisa hao kuweka mikakati madhubuti ya kusaidia jamii katika kuondokana na janga la udumavu kwa watoto wasiopata lishe bora ambalo lina madhara makubwa katika ukuaji wa mtoto. 

“Tafuteni mbinu ya kutoa elimu kwa jamii na ilete tija juu ya kumaliza  udumavu tuwe na  asilimia sifuri na haya yote yataletwa na mikakati madhubuti ya mtakayo kuwa mmeweka”, ameeleza Dkt. Mahera.  

Sambamba na hilo Dkt. Mahera amewataka watumishi wote kuheshimiana na kushirikiana ili sekta ya Afya itoe huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia miongozo ya utoaji wa Huduma za afya. 

Pia Mahera ameongeza kuwa  wafamasia wasimamie dawa kwa uangalifu ili wananchi wapate huduma na zenye uhakika kulingana na uwekezaji uliofanywa na serikali yao.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amezitaka Hospiatali za Rufaa nchini kuhakikisha zinatoa huduma za utengamao na tiba mazoezi ili kuwezesha wananchi wenye uhitaji wakiwemo watoto wenye ulemavu kuishi maisha yenye ubora na kuweza kujihudumia wao wenyewe

"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kununua vifaa tiba vya kisasa kuanzia ngazi ya msingi hadi taifa, ni lazima tuwe na mpango wa matengenezo, ili vikiharibika kidogo visiwekwe stoo kwani itakuwa ni hasara kwa serikali na kuwanyima wananchi huduma”, ameeleza Dkt. Grace


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.