• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Kinara wa UMITASHUMTA ang’ara kwenye UMISSETA

Imewekwa tar.: June 27th, 2021

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Mwanariadha Salma Charles Samwel wa Ushetu Kahama ambaye ni miongoni mwa wanafunzi 10 waliochaguliwa kujiandaa kushiriki mashindano ya kimataifa ya riadha huko Belgrade Serbia amedhihirisha ubora wake leo pale alipokimbia na wanariadha wanaoshiriki mbio za UMISSETA katika hatua ya robo fainali na kuwa wa kwanza

Salma ambaye alitamba katika mbio za mita 800 na mita 1500 kwenye  michezo ya UMITASHUMTA iliyomalizika hivi karibuni, leo alikimbia mbio za mita 1500 na kutumia dakika 4:46:13 huku akimwacha aliyeshika nafasi ya kwanza kwa wanafunzi wa sekondari Loema Itimay wa Manyara ambaye alikimbia mbio hizo akitumia dakika 4:52:41.

Akizungumzia kiwango cha mwanariadha huyo, Mratibu wa riadha wa UMITASHUMTA na UMISSETA Robert Kalyahe amesema Salma na wenzake 9 wanaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ya kimataifa.

Amesema kwa vile wanafunzi hao 10 wapo kambini Mtwara ameona ni vyema awashindanishe na wanafunzi wa sekondari ili aweze kuona hatua waliyoipiga tangu kuanza kwa mazoezi yao.

 Kalyahe anaamini wanariadha 6 watakaoshiriki mashindano ya kimataifa watafanya vizuri kulingana na program ya mazoezi wanayowapa wanariadha hao.

Mbali na Salma, mwanafunzi mwingine aliyeshiriki mbio za mita 1500 za UMISSETA hatua ya robo fainali ni Mwanaharabu Ally wa shule ya msingi Mtua wilayani Nachingwea ambaye alifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika kundi lake.

Naye mwanafunzi Damian Christian ambaye anasoma kidato cha pili katika shule ya sekondari ya St Patrick ya Arusha alitia fora kwenye mbio hizo za mita 1500 baada ya kuwaacha mbali wanafunzi wenzake.

Damian ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki UMISSETA mwaka huu ameonyesha umahiri mkubwa katika kukimbia mbio ndefu na anatamani kufikia rekodi ya wakimbiaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania kama Filbert Bayi na Juma Ikangaa.

Mchezo wa riadha ambao leo umeingia siku ya pili utaendelea kuchezwa kwa siku tano mfululizo ambapo baadhi ya michezo ipo ngazi ya hatua ya nusu fainali na fainali.

Katika mchezo wa kuruka miruko mitatu aliyeshinda kwa upande wa wanariadha wasichana ni Witnes Ibrahim wa Geita aliyeruka umbali wa mita 9:87 na kufuatiwa na Mwalu Madirisha wa Tabora aliyeruka umbali wa mita 9:62 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Eugenia Simon ambaye aliruka umbali wa mita 9.36.

Mchezo wa miruko mitatu kwa wavulana  mshindi ni Mussa Yusuph wa Shinyanga ambaye aliruka umbali wa mita 13:10, nafasi ya pili ilichukuliwa na Ewald Emanuel wa Manyara aliyeruka umbali wa mita 12: 90 na nafasi ya tatu imechukuliwa na Alphonce David wa Tabora ambaye aliruka umbali wa mita 12:60.

Kwa upande wa mchezo wa kurusha tufe wavulana mshindi wa kwanza ni Abdallah Salum wa Unguja ambaye alirusha umbali wa mita 14:30, nafasi ya pili ilichukuliwa na Edward Michael wa Dar aliyerusha tufe umbali wa mita 11:97, na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Rajab Mtonyi wa Dodoma ambaye alirusha umbali wa mita 11:42.

Mshindi wa mchezo wa kurusha tufe kwa wasichana anaitwa Keflonia Daudi wa Shinyanga kwa umbali wa mita 8:93, nafasi ya pili ilichukuliwa na Martha Matinga wa Simiyu kwa umbali wa mita 8:88 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Fatma Ussi Said wa Unguja  kwa umbali wa mita 8:70

 

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • REJESHENI MIKOPO ILI WENZENU WAPATE KUKOPA –KAMATI YA LAAC

    March 31, 2023
  • LAAC YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MTWARA

    March 31, 2023
  • KAMATI YA LAAC YAKAGUA MADARASA 7 YALIYOJENGWA KWA MAPATO YA NDANI NA NGUVU ZA WANACHI - MANISPAA YA SUMBAWANGA

    March 31, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.