Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Jafo Ataka Kasi ya Ujenzi Hospitali ya Gairo Iongezwe

Imewekwa tar.: March 22nd, 2019

Serikali imeuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kuhakikisha inaongeza kasi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Gairo ili kukamilisha kwa wakati kazi hiyo kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni Juni, 30 mwaka huu.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo alipofanya ziara wilayani Gairo kujionea ujenzi wa hospitali ya Gairo na kituo cha afya Gairo na kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri na wataalam wake kuongeza kasi ya ujenzi na kuzingatia viwango vya ubora na thamani halisi ya fedha.

“ninyi mpo nyuma mkilinganisha na wenzenu, wenzenu wengine nimekuta wapo mbali ninyi mpo nyuma, hapa kuna suala la maji kuwa yalikuwa hayapatikani lakini nimefurahi kusikia na mashine zimeongezwa, hapa vifaa vya ujenzi viongezwe, nia yangu ni kutaka kuona fedha iliyotumika inafanya kazi iliyokusudiwa na inakamilika kwa wakati, vifaa vyote vije hapa eneo la ujenzi“

Amewataka Wataalam kuzingatia maelekezo ya Serikali na kufanya kazi kama timu moja ili kuimarisha utendaji wao na kazi iliyokusudiwa hali wakizingatia thamani halisi ya fedha na kuepuka kumalizika kwa fedha kabla majengo hayajakamilika.

“Ninyi wataalam kazi yenu kubwa ni kuhakikisha viwango vinavyozingatia ubora na ujenzi vinafanyika, usitake Mhe. Mbunge au Mhe. Mkuu wa Wilaya aje akunyonyeshee kidole kwani ni wajibu wa Watendaji kuhakikisha kazi inakamika, Mkurugenzi hakikisheni kazi hii inakamika”

Aidha, amepongeza ujenzi wa kituo cha afya Gairo ambao umekamilisha majengo yote yaliyotakiwa kujengwa na kwamba ushirikiano wao uliopo uendelee na kuacha malumbano kama ilivyokuwa hapo awali kwani ushirikiano utaimarisha utendaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Gairo umeefikia asilimia zaidi ya 20 kwa sasa na watahakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana ili kukamilsha kazi kwa wakati kwa ajili ya kutoa huduma za afya mkoani Morogoro.

Dkt. Kebwe amesema Mkoa wa Morogoro ulipokea jumla ya shilingi bilioni 7.6 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya, bilioni 4.9 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya ambazo ni hospitali ya wilaya ya Gairo, wilaya ya Mvomero na wilaya ya Malinyi.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Gairo Dkt. Dastan Mshana amesema hadi kufikia tarehe 19 Machi mwaka huu jumla ya shilingi 200,471,567 zimekwisha tumika katika hatua za awali za ujenzi wa hospitali hiyo mpya ya wilaya.

Sirial S. Nchembe ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha na pia amemshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kufanya ziara za mara kwa mara na amesema amepokea maagizo ambayo watatekeleza mara moja  kama ilivyoagizwa.

Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Shabiby amewataka watendaji kufanya kazi kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha kama makusudio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwani inaitendea haki Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, “mimi niwakanye mfanye kazi inavyotakiwa kwa kadiri ya fedha zilizotolewa la sivyo hata mimi nitawabadilikia” ,

Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Gairo Bw. Shaban Sagilo amempongeza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuahidi kusimamia ujenzi wa hospitali mpaka utakapokamilika.

Aidha, Bw. Sagilo ametoa ombi la kupatiwa Jokofu la kuhifadhia maiti katika kituo cha afya Gairo ili kuwasitiri marehemu kwani ni changamoto ya muda mrefu hasa kwa uharibifu wa miili ya marehemu.

“tulikuwa tunaomba jokofu la kuhifadhia maiti (fridge) kituo cha afya Gairo ingekuwa ni jambo bora zaidi ili wale marehemu wetu waweze kukaa vizuri”

Halmashauri ya wilaya ya Gairo ni moja kati ya Halmashauri 67 ambazo zimepokea fedha kiasi cha shilingi bilioni moja na nusu, ujenzi wake wa awali ni majengo 7 ambayo ni jengo la kuhifadhi dawa, jengo la utawala, jengo la wagonjwa wa nje, maabara, wodi ya wazazi iliyounganishwa na jengo lake la upasuaji, jengo la kufulia, jengo la mionzi (X-ray).


                                  Anaandika Fred Kibano

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.