Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

KAIRUKI AWACHARUKIA VIONGOZI WA MKOA WA TANGA; WANAFUNZI ZAIDI YA 27,000 HAWAJARIPOTI KIDATO CHA KWANZA

Imewekwa tar.: January 17th, 2023

OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amekerwa na hali ya asilimia 55.2 ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Tanga kutoripoti shule.

Mhe. Kairuki ametoa kauli hiyo mkoani Tanga tarehe 16.01.2023 wakati akizungumza na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za  Sekondari, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi  na viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri  kwenye kikao kazi cha Uboreshaji wa Usimamizi wa Elimumsingi na Sekondari katika shule ya sekondari Tanga ufundi.

Amesema takwimu za wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza si ya kuridhisha katika mkoa huo.

“Ukiangalia kwenye elimu ya awali mpaka sasa uandikishwaji ni asilimia 82 , lakini nilitamani nisikie kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ni asilimia ngapi ili nao tusiwaache nyuma.”

“Kwa upande wa uwandikishwaji wanafunzi darasa la kwanza mmefikia asilimia 87.7 lakini changamoto inakuja kwenye kuripoti wanafunzi wa kidato cha kwanza.”

Amesema mpaka Januari 13, mwaka huu zaidi ya wanafunzi 27,867 ambao ni sawa na asilimia 55,2 hawajaripoti shule huku walioripoti kwa Wilaya ya Kilindi ni asilimia 11 pekee.

Mhe. Kairuki amesema mpaka sasa ni asilimia 44.8 pekee ya wanafunzi ndio wameripoti shule katika mkoa huo na kusisitiza kuwa ni lazima kila kiongozi kuhakikisha takwimu hizo zinabadilika ndani ya muda mfupi.

Amesema kati ya wanafunzi 27,867 ambao hawajaripoti shule, asilimia kubwa imechangiwa na Wilaya ya Kilindi ambayo ni asilimia 11 pekee ndio walioripoti huku Korogwe Mji ikiwa ni asilimia 22.78,  Korogwe TC asilimia 30.21, Handeni TC asilimia 42.55, Handen DC asilimia 45.86, Bumbuli asilimia 53.26, Mkinga asilimia 27.98 Muhenza asilimia 50 Pangani 52 na Tanga jiji 76.23

“ Je hii ni sawa jamani? Hivyo kila mmoja kwa kadri inavyowezekana takwimu hizi zibadilike ndani ya muda mfupi sana. Haiwezekani tupo siku 16 ya mwezi wa kwanza na watoto zaidi ya 27,867 hawajaingia shule. “

“Kila mmoja arudi, ajitafakari kwa vitendo tufanye tathimini sahihi ya kufuatilia mtoto mmoja baada ya mwingine na bahati nzuri sana wengi wa wanafunzi wanatoka mkoa huu huu na wanatoka kwenye meneo yetu  ambako tuna waratibu wa Elimu kata, Maafisa Elimu halmashauri,  rudini katika orodha angalieni nani yuko wapi na kwa nini hajafika shuleni.”

Amesema takwimu zinaonesha kuwa Wilaya ya Lushoto ni ya mwisho katika uandikishaji wa elimu ya awali huku Pangani ikiwa na asilimia 48 na Korogwe DC ina asilimia 67 na kusisitiza haja ya kubadilika,

“Angalau tungekuwa bado mwezi mmoja kufungua shule lakini tayari watoto wamesharipoti  siku saba sasa, na ukomo tuliojipangia tayari siku 16 zimepita je unatarajia ni nani ashuke afanye uhamasishaji wa uandikishaji kama sip nyie?”

Amesema kitendo cha watoto kutoandikishwa na kutoripoti kidato cha kwanza kunaondoa maana ya juhudi za Serikali za kujenga madarasa.

“ Haya madarasa tuliyoyajenga yatakuwa na maana gani, maamuzi yote tuliyofanya ya kisera yatakuwa na maana gani endapo watoto zaidi ya 27,000 ni watoto wengi sana kuwa nyumbani.”

Aidha, Mhe. Kairuki amesema kuwa masuala ya uandikishwaji wanafunzi na kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza pia amekuwa akitumia kutafsiri utendaji wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi.

“ Mimi hizi nazitafsiri kwenye maeneo mengi, ninyi mnaweza mkaona naangalia kwenye elimu peke, inanisaidia kutafsiri kuanzia Wakuu wa Willaya na pia naangalia Wakurugenzi tulionao, shida ni nini?

“ Haya ni maeneo mengine kati ya yale 12 ya mkataba wetu wa utendaji.”

Mhe. Kairuki amesema pia kwa upande wa ufaulu wa darasa la saba na kidato cha pili, bado Tanga haifanyi vizuri na kuwataka viongozi wajitafakari kilichotokea.

“Ndugu zangu tusipobadilika tutakuwa tunamvunja moyo Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali. Rais amechukua hatua mbalimbali za kitumishi kushughulikia changamoto nyingi na kuboresha sekta ya Elimu.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.