• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Jinsi Milioni 540 zilivyobadilisha uchumi wa Wanawake, Vijana na Walemavu Ilemela

Imewekwa tar.: February 11th, 2021

Na Violencea S. Mbakile, Mwanza

Kiasi cha sh 540,000,000 ambazo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela zilitosha kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa vikundi 166 vya wanawake, vijana na walemavu katika halmashauri hiyo katika mwaka wa fedha 2019/2020.

Katika fedha hizo vikundi 126 vya wanawake vilipatiwa kiasi cha Shilingi 418,000,000, vikundi 32 vya vijana vilipatiwa shilingi 101,000,000.00 na Shilingi Milioni 21,000,000 zilitolewa kwa vikundi 8 vya walemavu.

Kutolewa kwa fedha hizo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu katika halmashauri ya Wilaya ya Ilemela kwa mwaka 2019/2020 ni ukombozi wa pekee kwa makundi haya katika jitihada zao za kujiletea maendeleo na kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini.

Katika kipindi cha miaka mitano yaani kuanzia 2015 hadi 2020 jumla ya Shilingi 1,431,000,000 zimetolewa kwa vikundi 414 vya wanawake, vikundi 112 vya vijana na vikundi 13 vya walemavu ambapo wao walihudumiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Ili kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa malengo tarajiwa, wataalamu kutoka idara ya maendeleo ya jamii ya Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na madiwani wa viti maalum, huhakikisha kwanza wanawajengea uwezo kwa kuwapa elimu na mafunzo mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya fedha hizo.

Vikundi vingi vinavyopatiwa mikopo hiyo hujishughulisha na shughuli za ushonaji, utengenezaji wa batiki,sabuni za maji, kilimo cha bustani, biashara ya dagaa na samaki , ufugaji na shughuli za uchomeleaji

Kikundi cha vijana kinachojulikana kama mafundi welding ni mojawapo ya kikundi kinachofaidika na mkopo huu kutoka Halmashauri kilichopo Kata ya kirumba na hujishughulisha na shughuli za kutengeneza milango, madirisha pamoja na nanga za vyombo vya majini

Alex Stephen ambae ni katibu wa kikundi cha vijana mafundi welding anaeleza kuwa mkopo huu umewasaidia sana kwani walianza na mtaji wa kiasi cha shilingi laki tano lakini hadi kufikia sasa mtaji wao umefikia kiasi cha Shilingi Milioni tatu za kitanzania.

 “Tulianza kazi zetu kwa kusuasua, kwa mtaji mdogo wa mashine moja ya thamani ya shilingi laki tano, ambayo wote tulikuwa tunaitegemea katika kufanya kazi ambapo ilitulazimu kusubiriana lakini baada ya kupata mkopo awamu ya kwanza wa kiasi cha shilingi milioni mbili mambo yalibadilika,” amesema Stephen.

 Kulingana na Stephen na mkopo huo umewafanya  kupiga hatua moja kwenda nyingine mpaka sasa wana jumla ya mtaji wa shilingi milioni tatu na wanazo mashine nne za kuchomelea tofauti na awali walikuwa nayo moja tu hivyo kusababisha kuchelewesha kazi za wateja wao.

Ameishukuru serikali ya kata kwa kuunga mkono shughuli zao mfano zinapotokea zabuni hushirikishwa huku akitoa ushuhuda kuwa wamepewa kazi ya kutengeneza madirisha ya shule ya sekondari Kirumba hii ni moja ya hatua mpaka sasa.

Naye Mwenyekiti Msaidizi wa kikundi cha wakinamama malengo kutoka kata ya Buswelu Veronica Pole amesema kuwa kikundi chao hujishughulisha na ujasiriamali wa biashara ya kuuza pochi, vikapu na sabuni kwa matumizi ya nyumbani ambapo husambaza ndani ya Mwanza na nje ya Mwanza.

Amesema kuwa walianza na mtaji wa kiasi cha shilingi laki nane na kufanikiwa kununua vifaa vyote lakini ambapo hadi sasa wamefikisha mtaji wa milioni mbili tofauti ambayo ni tofauti na mkopo wanaopata hivyo ukiweka na halmashauri mtaji umekuwa na kufikia shilingi milioni nane.

“Tunaishukuru halmashauri ilitukopesha milioni mbili laki tano tukarejesha ikatuongezea tena milioni nne na wenyewe tumeweza kuurejesha, mara ya kwanza tulikuwa tunarejesha kwa riba lakini sasa hivi hatulipi riba, Kwa ushauri kwa mkopo tunaomba watuongezee tutakapoomba tena mkopo ili tupate kikubwa zaidi maana tunampango wa kufungua biashara kubwa zaidi tunataka tuwe wakala wa mpesa na mabenki ili tuwe na mradi mwengine,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha walemavu Maendeleo Nyakato Veronica Mtilo ameeleza  kuwa kupitia mkopo huu wameweza kununua mashine kubwa ya kushona masweta yenye thamani ya Shilingi Milioni saba hii ni baada ya kumaliza kulipa mkopo wa awamu ya kwanza huku wakiiomba serikali iendelee kuwasaidia watu wenye ulemavu maana wameweza kuwa na shughuli za kufanya na kuaacha kuomba omba.

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana kupitia mikopo hii zipo changamoto mbalimbali ambazo Halmashauri imekuwa zikikabiliana nazo katika suala hili la utoaji wa mikopo ambazo ni pamoja na baadhi ya vikundi kutokurejesha mkopo kwa wakati, vikundi vingi vya vijana vinavyopata mkopo huu husambaratika hivyo kupelekea kutokurejesha mkopo.

Kwa upande wa vikundi vya walemavu wamekuwa wakidhani mkopo huu ni ruzuku hivyo hawarejeshi kabisa au hurejesha kwa kusuasua hivyo.

Vikundi vingine hubadili matumizi ya mikopo tofauti na miradi waliyoombea hivyo kupelekea kutofikia malengo yaliyotarajiwa.

Ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imejiwekea mikakati mbali ya kuhakikisha kuwa fedha hizi zinaendelea kuwanufaisha makundi haya na kuweza kujikwamua kiuchumi baadhi ya mikakati hiyo ikiwemo ni ufuatiliaji wa marejesho ambapo ipo timu maalum ya ufuatiliaji inayohusisha wataalam wa maendeleo pamoja na madiwani wa viti maalum ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwapa elimu ya urejeshaji wa mikopo.

Ipo mikakati mbalimbali ambayo imewekwa katika kuhakikisha kuwa makundi haya yanawezeshwa na kujikwamua na suala zima la umaskini ikiwemo kuhakikisha kuwa makundi haya yanapewa mkopo mkubwa katika kila kata ambao utawawezesha kutekeleza mradi mkubwa ambao utakuwa wa mfano kwa jamii, pia kuendelea kutoa mikopo midogo midogo kwa makundi hayo.

Mikakati mingine ni pamoja na kuwa Halmashauri imejipanga kutenga eneo kwa ajili ya kuwawezesha vijana kutekeleza shughuli zao za kiuchumi ili kuweza kujikwamu na suala la umaskini, pia ni kuendelea kuhamasisha vikundi hivyo juu ya kuwa na miradi iliyo kwenye muundo wa viwanda.

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.