• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Jiji Dodoma watakiwa kuandaa mkakati wa kutangaza uwekezaji

Imewekwa tar.: January 28th, 2019

Uongozi wa Jiji la Dodoma umetakiwa kuandaa mpango mkakati wa kutangaza maeneo ya biashara na uwekezaji hususani ni miradi inayoendelea kujengwa ya soko kuu na kituo kikuu cha Mabasi jijini Dodoma.

Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Jiji la Dodoma.

“Sasa hivi andaeni utaratibu maalum wa kutangaza miradi hii ambayo itakamilika hivi karibuni, kama ni Kampuni itakayosimamia na kuendesha miradi hii au utaratibu wowote mtakaoona unafaa ili mradi miradi hii iweze kuongeza mapato ya Jiji letu” alisema Jafo.

Sio miradi hii inakamilika ndio mnaanza kutafutana hamjui nini cha kufanya, mnatakiwa muanze kujipanga kuanzia sasa namna gani miradi hii itajiendesha kibiashara na kuleta faida kubwa zaidi, alisema.

Aidha ameongeza kuwa hili ndio litakua soko la pili la kimataifa baada ya kariakoo na na hili litakua la kisasa na bora  zaidi kwa kuwa limejengwa kukidhi mahitaji ya wakazi wa makao makuu ya Nchi na linaendana na hali ya sasa hivyo linahitaji uongozi makini utakaoweza kulisimamia na kuliendasha kwa faida.  

Kwa kuongezea Jafo ametoa wito kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi kudumisha ushirikiano katika kusimamia miradi ya umma ili kuleta maendeleo chanya katika jiji la Dodoma kwani ushirikiano ndo silaha kubwa katika kutekeleza uongozi wowote.

Awali ya yote Jafo ametoa pongezi kwa Kampuni ya Mohammed Builders, Kampuni  ya hapa nchini ambayo inafanya vizuri katika ujenzi wa miradi mbalimbali waliyopewa kuitekeleza katika Jiji la Dodoma kupitia mradi wa mpango miji mkakati unaotekelezwa kupitia fedha za mkopo toka Benki ya Dunia.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa yeye na watendaji wake wako imara katika kusimamia sheria,taratibu na kanuni za nchi ili kuongeza chachu ya maendeleo katika jiji la Dodoma.

Mhe. Katambi amesema kuwa yeye na timu watahakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo vyema na kukusanya kwa makini mapato ya jiji; Pia watahakikisha mapato hayo yanatumika kuleta maendeleo kwa wana Dodoma na watanzania kwa ujumla kwani Dodoma ndo makao makuu ya Nchi hii.

“Mh.Waziri nikuombe unifikishie salamu zangu kwa Mh.Rais kuwa Dodoma pako salama na wala hakunamigogoro katika uongozi wetu na tunatekeleza majukumu yetu kwa makini  na kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ” Amesema Katambi.

Kwa kuhitimisha Mkurugenzi wa Jiji Godwini Kunambi amesema kuwa Jiji wamejipanga ifikapo 2021 panapo majaaliwa  jiji la Dodoma linaweza kujitegemea kwa mapato bila kutegemea ruzuku toka Serikali Kuu.

“Mh.Waziri ili tuweze kufikia malengo ya jiji 2021 kuweza kujiendesha lazima tuwe na kampuni ya jiji itakayoweza kusimamia na kuendesha miradi yote itakayokuwa ikitekelezwa ndani ya jiji letu na nikuhaidi kuwa tutatekeleza vyema maagizo yako.”

Kunambi alimalizia kuwa sisi kama Jiji jukumu letu kubwa ni kutoa huduma kwa wananchi hivyo ili miradi hii iweze kufanya biashara tutaanzisha Kampuni kama tulivyoelekezwa, ambayo itakua inajitegemea na itahusika na uendeshaji wa shughuli zote za maeneo ya biashara kama hili soko la kimaita, stendi ya mabasi, stendi ya Malori na maeneo mengine ambayo yatakidhi kutoa huduma za kibiashara Aliongezea Kunambi.

Katika zaira yake ya siku moja Mhe. Jafo alitembelea na kukagua ujenzi wa stendi ya malori Nala, ujenzi wa kituo afya Mkonze, ujenzi wa Soko la kimataifa Nzuguni pamoja na ujenzi wa stendi ya kisasa


Matangazo

  • Orodha ya Majina ya Waliopata Ajira Kada za Afya na Elimu Juni 2023 June 05, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.