Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Jafo: Wizi wa mitihani unaporomosha elimu

Imewekwa tar.: September 30th, 2019

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amekema tabia ya wizi na udanganyifu wa mitihani na kusema kuwa jambo hilo limekuwa likiporomosha elimu ya Tanzania.

Ameyasema hayo leo wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa kwanza wa Wenyeviti wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara kutoka  katika Halmashauri zote nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Amesema wizi wa mitihani sio sifa njema kwa Taifa na umekuwa ukiporomosha Taifa katika suala la elimu na kuwaonya walimu kutojihusisha na vitendo vya kushiriki kufanya njama ya udanganyifu.

“ Sio jambo jema kabisa, kuna wanafunzi wanafaulu sana na kuchaguliwa kwenda kwenye shule za vipaji, lakini wakifika huko utashangaa kama kweli alifaulu na hii inatokana na tabia ya wizi na udaganyifu wa mitahani jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu nchini.

Mhe. Jafo amesema udanganyifu wakati wa mitihani na wizi wa mitihani, vimekuwa na athari kubwa kwa mtu mmoja mmoja kwa maana ya mwanafunzi, mwalimu, shule na taifa kwa ujumla hivyo ni vyema tabia hii ikafika mwisho.

Amewataka walimu wakuu hao kuhakikisha  wanasimamia kanuni na weledi kwenye masuala ya mitihani ili kuunga mkono juhudu za Serikali za kutaka kutoa elimu bora kwa jamii na kuinua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi.

Amewashukuru Baraza la Mitihani nchini  kwa kusimamia nidhamu katika usimamizi wa mitihani kwa sasa jambo ambalo limesaidia kupunguza  wizi wa mitihani ambapo lilikuwa likiigharimu Taifa.

 “Niwasihi nyinyi mliopewa dhamana katika hili, nendeni mkafanye utekelezaji wa suala zima kwa kuzingatia kanuni na kusimamia weledi kwenye usimamizi wa mitihani nchini.”Amesisitiza Mhe. Jafo

Kuhusu kutambua mchango wa walimu wanaofanya vizuri katika mtihani nchini Mhe. Jafo amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itatoa tuzo ya ufanyaji vizuri wa mitihani ili kuleta motisha kwa walimu na wanafunzi kuanzia mwaka huu.

Vilevile amesema kuwa uimarishaji wa miundombinu umekuwa ni mkubwa ambapo lengo la Serikali ni kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata fursa ya elimu na kusoma katika mazingira mazuri.

Amesema pamoja na fedha zinazotolewa kwa ajili ya elimu bila malipo, Serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni 305.1 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa, matundu vya vyoo, maabara na maboma.

Mhe. Jafo ameendelea kusema kuwa kwa mwaka huu, Serikali imetenga Sh bilioni 288.247 kwa ajili ya elimu bila ya malipo kukiwa na ongezeko la kibajeti ukilinganisha na mwaka uliopita.

 “Ajenda ya elimu kwa sasa inaenda kwa kasi sana, bajeti ya mwaka huu tumetenga sh bilioni 288.247, katika program ya elimu bila malipo na kutoa zaidi ya Sh bilioni 24 kila mwezi, ikiwamo sh bilioni 3.2 ambazo ni kwa ajili ya posho za walimu.

Mhe.Jafo amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika shule za kata ili wanafunzi waweze kupata elimu bora.

Wakati huohuo, Mhe Jafo amesema Serikali ilibainisha shule kongwe 89 ambazo zilikuwa katika hali mbaya lakini  mpaka sasa shule 43 tayari zimekabidika kwa  kufanyiwa maboresho huku zilizobaki zikiwa katika hatua mbalimbali za maboresho.

Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wakuu wa shule za msingi Tanzania bara(Tapsha), Rehema Ramole, amesema umoja wa waalimu shule za msingi umesikitishwa na baadhi ya walimu ambao wanaojihusisha na udanganyifu kwenye mitihani ya darasa la saba.

“Tunasikitishwa na tabia ya baadhi ya walimu kushiriki kwenye wizi na udanganyifu wa mitihani ya darasa la saba kwa lengo la kutaka kupata ufaulu mzuri, ni vema walimu tukajiepusha na hili.”Amesema Bi. Ramole

Bi. Ramole ameipongeza Serikali kwa kuipa kipaombele sekta ya elimu na kuahidi kuendelea kushikamana bega kwa bega ili kuhakikisha yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi yanatekelezwa.

Aidha ameipongeza Serikali kwa kuwalipa walimu mshahara kwa wakati, kulipa malimbikizo ya posho na madai mbalimbali, sambamba na kulipwa Sh 200,000 kama posho ya madaraka kwa walimu wakuu na kupandishwa madaraja.

Na. Angela Msimbira OR- TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Fomu za kujiunga na Kidato cha kwanza 2024 December 16, 2024
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.