• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

JAFO: Nitawatetea madaktari wanaotimiza wajibu wao.

Imewekwa tar.: August 20th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema kuwa atawatetea madaktari ambao watatimiza majukumu yao lakini hatasita kuwachukulia hatua wale ambao wataenda kinyumbe na taratibu.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya leo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema kuwa madaktari wamekuwa wakijitoa kwa weledi mkubwa katika kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa jamii na kuleta mabadiliko katika sekta ya afya  nchini.

“kuna watu wanafanyakazi usiku na mchana  tusipowalinda watu wanaofanyakazi  tutawaumiza,  siamini kama kweli mtumishi mmoja pekee anaweza kula fedha bila kuwa na ushirikiano na watu wengine, si kweli hata  kidogo, tutende haki kwa watumishi wanaotoa huduma za afya nchini” Amesisitiza Mhe. Jafo

Amesema Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanaofanya vibaya wanapaswa kuadhibiwa lakini lazima haki itendeke katika kuwachukulia hatua ili kuleta usawa na kupunguza malalamiko kwa wataalam wa afya nchini.

Amewaagiza viongozi wa Halmashauri kutenda haki wakati wa kuwachukulia hatua watumishi kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma na kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kina wa tuhuma zilizotolewa dhidi yao ili kujiridhisha ndipo watoe maamuzi  yaliyosahihi.

Mhe. Jafo anafafanua kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kuwashusha madaraka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya  bila kufuata sharia na taratibu za kiutumishi kwa kusikiliza majungu na uongo usiofanyiwa kazi jambo hili si haki, hivyo serikali itaendelea kuwatetea na kuhakikisha wanarudishwa kwenye nafasi zao.

Naye,  Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa Serikali imejenga miundombinu ya  huduma za afya ambapo  mpaka sasa vituo 470  vimekarabatiwa na kujengwa nchini  kwa gharama ya shilingi  bilioni 321.

Mhandisi Nyamhanga amewaagiza Wanganga Wakuu wa Mikoa na Wiilaya kuhakikisha wanasimamia utoaji wa huduma bora za afya kwa watumishi ili waweze kufanyakazi kwa bidi na kuhakikisha huduma za afya zinaboreka nchini.

Wakati huohuo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo na Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndungulile amewataka Wanganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha watumishi walio chini yao wanatoa huduma bora kwa jamii ili kuwavutia kupata huduma  hiyo kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya vilivyojengwa nchini.

Aidha Katibu Mkuu wa Afya, Maendeleo na Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula amewataka  Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya  nchini kuhakikisha wanafanyakazi kama timu kwa kudumisha umoja na ushirikiano ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa jamii zinakuwa bora nchini.

 Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA

    January 23, 2023
  • MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA DODOMA JIJI KWA UWEKEZAJI

    January 20, 2023
  • SERIKALA YASISITIZA KILA MMOJA KUTUNZA MAZINGIRA

    January 20, 2023
  • TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKANA NA WADAU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    January 20, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.