Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Jafo ahoji Mil 60 ununuzi wa dawa ya mchwa Hospital ya Wilaya Morogoro Dc

Imewekwa tar.: July 12th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) amehoji matumizi ya shilingi mil 60 manunuzi ya dawa ya mchwa katika jengo la Hospital ya Wilaya ya Morogoro linaloendelea kujengwa katika eneo la Mvuha.

Mhe. Jafo alihoji matumizi hayo baada ya kutoonekana kwa kipengele hicho kwenye taarifa ya matumizi za fedha za ujenzi wa hospital hiyo pamoja na gharama kubwa iliyotumika kununulia dawa hizo.

Akiwa katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa hospital za Wilaya ya Morogoro Mhe. Jafo alipokea taarifa ya ujenzi yenye mchanganuo wa matumizi ya fedha zaidi ya Tsh Bilioni moja ilihali kipengele cha ununuzi wa dawa hizo za mchwa uliotumia zaidi ya Shilingi mil 60 kutoonekana kwenye matumizi yaliyowasilishwa.

Mhe. Jafo alihoji endapo dawa ya kudhibiti  mchwa iliwekwa kwenye majengo hayo na kujibiwa kuwa ndio na kazi hiyo ilifanyika kwa gharama ya shilingi milioni 60 ndipo alipouliza kwanini matumizi ya fedha  hizo hayajawekwa kwenye taarifa.

“Bei ya ununuzi wa dawa hiyo si halisi na sijui kama mlijaribu kujilinganisha na wenzenu wa halmashauri nyingine ili mfahamu kuwa  walitumia kiasi gani kwenye ununuzi wa dawa kama hiyo ni kiasi gani au ninyi mmenunua dawa ya aina gani ambayo imegharimu kiasi hiki kikubwa cha Fedha” Alihoji Jafo

Jafo aliongeza kuwa kama mlinunua dawa hiyo kwanini matumizi ya fedha hizo hayaonekani kwenye taarifa yenu, napata mashaka na matumizi ya fedha hizo hapa ni lazima ije Timu maalumu kwa ajili ya kuchunguza matumizi mabaya ya fedha za Mradi wa Ujenzi wa Hospitali hii aliongeza Jafo.

Wakati huo huo Jafo alisema kuwa kwa kipindi kirefu halmashauri ya Morogoro Dc imekuwa na matumizi yasiyoridhisha ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo hali hiyo inaonyesha dhahiri kuwa kuna changamoto ya kiungozi.

“Hapa kuna tatizo kubwa na lazima tulipatie ufumbuzi haiwezekani nyie mara mnashindwa kutekeleza miradi kwa wakati kuanzia ujenzi wa Jengo la Halmashauri shilingi milioni 500 hazijulikani zilipo na mpaka leo Jengo halijajengwa sasa mnataka tena tabia hiyo muilete kwenye mradi wa Hospital safari hii mtamaliza ujenzi huu haijalishi fedha mnazo au mmezitumia ni lazima mkamilishe ujenzi.

Mpaka sasa mmekwishatumia shilingi Bil 1 kujenga majengo haya ambayo hayaridhishi hna hamjafikia hata kwenye hatua ya kupaua huku mnaniambia mmebakiwa na shilingi milioni 400 sitaki kusikia sababu yeyote ninachotaka ni kuona ifikapo Julai 30 Hospital hii imekamilika” Alisema Jafo.

Akitolea ufafanuzi changamoto zilizojitokeza katika ujenzi wa hospital ya Wilaya  Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama imekuwa ikishauri kila wakati namna bora na ya haraka ya kukamilisha mradi huo lakini kumekua na muitikio mdogo wa wataalamu wa Halmashauri katika kutekeleza yale yanayoshauriwa na Kamati hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Morogoro Dc Masoud Rioba alifafanua manunuzi ya dawa za kuua Mchwa kuwa yalijumuishwa kwenye taarifa ya mradi katika kipengele cha vifaa vya ujenzi na sio kwenye kipengele kinachojitegemea ndio maana sio rahisi kuiona kwa uharaka.

“Manunuzi ya dawa yamejumuishwa kwenye vifaa vya ujenzi haionekani kwa haraka kwa sababu hatukuiweka peke yake na gharama yake ni shilingi mil 60 hii ni  baada ya kununua lita 1500 ambazo ndizo zilizokuwa zinahitajika na kila lita moja ilikua na gharama ya zaidi ya shilingi elfu 55 hivyo kuleta gharama ya zaidi ya shilingi milioni sitini” Alisema Rioba

Akifafanua kuhusu fedha zilizobakia kama zinaweza kukamilisha ujenzi wa Hospital hiyo amesema mpaka sasa vifaa vingi vimekwishanunuliwa hivyo fedha hiyo iliyobakia itaweza kufanya kazi za ukamilishaji wa majengo hayo na amemuhakikishia Mhe. Waziri wa Nchi kuwa kazi hiyo itakamilika kwa fedha zilizobakia.

Wakatihuo huo mmoja wa mafundi wanaotumika katika kazi za ujenzi wa hospital hiyo amelalamika kukosekana kwa vifaa vya ujenzi kwa muda mrefu katika Hospitali hiyo huku malipo ya mafundi hao yakisuasua kitu kilichoplekea  kuwakatisha tamaa na morali wa kuendelea kufanya kazi hiyo.

Mbali na changamoto zote hizo zilizojitikeza Waziri Jafo ameagiza uchunguzi ufanyikemara moja wakati huo huo kazi ya ujenzi ikiendelea na Uongozi uhakikishe  ujenzi wa hospital hiyo ifikapo Julai 30, 2019.



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.