Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Hoja za ukaguzi mwisho 30, Juni 2018: Serikali

Imewekwa tar.: May 5th, 2018

Serikali imeziagiza Sekretarieti za Mikoa kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa kukamilisha majibu ya hoja zote za ukaguzi za mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017, na kuwasilisha majibu hayo kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya uhakiki kabla ya tarehe 30 Juni, 2018.

Maagizo hayo yametolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Ndugu Tixon Nzunda, wakati akifungua kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi kutoka Seksheni za Mipango na Uratibu, pamoja na Makatibu Tawala Wasaidizi wa Seksheni za Usimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Sekretarieti za Mikoa, kilichofanyika Mei 4, 2018 katika Ukumbi wa Video Conference, OR-TAMISEMI.

Ndugu Nzunda ameyasisitiza hayo kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, kuwa Mikoa yote ni lazima sasa ijipange kuhakikisha inasimamia ipasavyo kazi ya kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili ifikapo muda uliotolewa na Serikali hoja zote za ukaguzi ziwe zimejibiwa ipasavyo na kuwasilishwa katika mamlaka husika.

Mbali na kuwaagiza kusimamia ipasavyo suala la kujibu hoja, Naibu Katibu Mkuu aliwaambia Makatibu Tawala  hao wasaidizi  juu ya mwenendo wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo alisema kuwa bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa iliandaliwa kupitia mfumo wa PlanRep iliyoboreshwa (PlanRep Web Based), ambao umewezesha Halmashauri zote 185 kuwa namipango iliyoboreshwa.

Ndugu Zunda amewataka watendaji pia kusimamia kazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo iliyopo bila ya kuwaonea haya Wakurugenzi wa Halmashauri.

“Mkurugenzi kwa mujibu wa utendaji anawajibika kwa RAS, na wewe unapotekeleza majukumu yako unakuwa umevaa kofia ya RAS, hivyo sitegemei Katibu Tawala Msaidizi katika ngazi ya Mkoa atoe visingizio kuna Mkurugenzi anamkwamisha katika kutekeleza wajibu wake,” alisema Ndugu Nzunda, na kuongeza kuwa katika awamu ya sasa hakuna wa kuachwa kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.

Naibu Katibu Mkuu amefafanua kwamba,  kikao hicho watajadili kwa kina vipaumbele vya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2018/19 ambavyo ni pamoja na kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za Afya, Elimu na Maji, kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri, kuanzishwa kwa fursa za miradi ya kimkakati, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, majengo ya utawala kwa Halmashauri mpya, sambamba na ununuzi wa magari ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya.

Maeneo mengine ya Bajeti ni ununuzi wa boti za kutolea huduma kwenye maeneo yenye changamoto za usafiri wa majini, kutenga maeneo ya uwekezaji, hususan viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, sambamba na kutenga fedha kwa ajili ya vijana na akina mama na watu wenye ulemavu, huku nguvu kubwa ikiwekwa katika sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi naukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akitoa maelezo ya awali, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa, OR TAMISEMI, Bibi Beatrice Kimoleta alisema kuwa Seksheni ya Mipango na Uratibu pamoja na Seksheni inayosimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa ni viungo muhimu katika suala zima la masuala ya mipango na bajeti.

“Lazima mtambue kwamba hizi idara mbili ninyi ndio injini ya Katibu Tawala Mkoa katika kumshauri juu ya masuala mazima ya mipango na bajeti. Kamwe huwezi kuzitenganisha idara hizi halafu ukafanikiwa, hivyo shabaha ya kuwaleta pamoja katika kikao hiki ni kutaka muwe na uelewa wa pamoja ili mtakapotoka hapa mkalete matokeo chanya kwenye Mikoa na Halmshauri zenu,” alisema Kimoleta.

“Katika mwaka wa fedha 2018/19, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepanga kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 6,186,418,709,500. Kati ya fedha hizo, shilingi 298,346,001,000 ni kwa ajili ya Sekretarieti za Mikoa sawa na asilimia 5% na Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetengewa shilingi 5,888,072,708,500 sawa na asilimia 95%” alisema Nzunda.



(Picha na habari na Atley Kuni)

Kwa Habari na picha Zaidi tembele  hapa  http://blog.tamisemi.go.tz/hoja-za-ukaguzi-mwisho-30-juni-2018-serikali/


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.