• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Halmashauri zisizotoa 10% kwa Vikundi Kukiona

Imewekwa tar.: April 12th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani S. Jafo(Mb) amewataka  Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha wanatoa mikopo kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Walemavu kutoka katika asilimia kumi ya mapato ya ndani kama ilivyoelekezwa kwenye Sheria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake asubuhi ya Leo Mhe. Jafo amesema Halmashauri zitakazoshindwa kutoa mikopo kwa vikundi hivyo watachukuliwa Hatua kali za kisheria kama ilivyoelekezwa katika Kanuni za utoaji wa mikopo ya vikundi.

Amesema kuwa licha ya uwepo wa Sheria  inayoelekeza suala zima la Utoaji wa mikopo kwa vikundi, utekelezaji wake  umekua wa kusuasua sana kwa baadhi ya Halmashauri na hadi kufikia Machi 2019 jumla ya fedha zilizotolewa kwa vikundi ni shilingi bilioni 20.7 ya shilingi bilioni 54.08 zinazopaswa kutolewa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 sawa na asilimia 38.27 ya Lengo.

“Hivi sasa hakuna kisingizio chochote katika utekelezaji wa sheria hii kwani Serikali imeshatoa Kanuni, zinazoongoza utoaji wa mikopo hiyo na Kanuni hizo zimetangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 141 la Tarehe 5 April, 2019 kwa GN. Na. 286 la mwaka 2019 kwa hiyo Mkurugenzi atakayeshindwa kutekeleza kwa ufanisi atachukuliwa hatua” alisema Mhe. Jafo.

Aliongeza kuwa katika kipindi hiki kuna Halmashauri 23 ambazo zimefanya vibaya zaidi kwa kutoa mikopo chini ya asimili 20 ya malengo.

Amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni Nsimbo, Nyasa, Busega, Kondoa Dc, Namtumbo, Kasulu Dc, Bariadi Dc, Msalala, Mbulu Tc pamoja na Njombe Dc.

Halmashauri zingine ni  Kongwa Dc, Musoma MC, Sumbawanga Dc, Kondoa Tc, Uvinza Dc, Ilala Mc, Lindi Dc, Mpwapwa Dc, Bahi Dc, Chamwino Dc, Momba Dc, Temeke Mc, Mbulu Dc na Lindi Mc.

Wakati huo huo Mhe. Jafo alitoa maelekezo kwa Halmashauri zote kuwa zinapaswa kutoa fedha kwa vikundi kwa mujibu wa Sheria na mpaka  ifikapo Juni 30,2019 Halmashari  ziwe zimetoa mikopo siyo chini ya asilimia 83 ya fedha zote za mikopo kutoka asilimia 10 ya fedha zote za mapato ya ndani.

Ameoongeza kuwa mpaka ifikapo Julai 20, 2019 Halmashauri zote ziwe zimetoa mikopo yote kwa asilimia 100 ya  fedha zote za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

“Mkurugenzi yeyote atakayeshidwa kutoa fedha kwa Vikundi kama ilivyoanishwa hapaswi kumlaumu mtu yeyote kwa sababu atachukuliwa hatua kama ilivyo elekezwa kwenye Kanuni za utoaji wa mikopo ya vikundi” amesema Mhe. Jafo.

Ikumbukwe kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya marekebisho katika Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura Na, 290 katika kifungu 37A ambacho kimeelekeza namna ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu kutoka katika asilimia 10 ya mapato ya ndani.


Mwisho.

Matangazo

  • Orodha ya Majina ya Waliopata Ajira Kada za Afya na Elimu Juni 2023 June 05, 2023
  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.