Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Halmashauri Zakusanya Bil 449 Mapato Ya Ndani

Imewekwa tar.: April 26th, 2019

IKIWA imepita robo tatu ya mwaka wa fedha 2018/2019, halmashauri zote zimekusanya Sh bilioni 449.8 ambayo ni asilimia 61 kati ya Sh bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo vya ndani huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkoa wa Dar es Salaam zikiongoza kwa mapato ghafi.

Hayo yabamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alipokuwa akitoa taarifa za makusanya kwa halmashauri kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu na kusisitiza kuwa vyanzo vya mapato vinavyokuswanywa na serikali kuu havijumuishi katika makusanyo hayo.

Akifafanua zaidi Jafo alisema halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi(asilimia 113), Geita (asilimia 109), Wanging’ombe(asilimia 105), Kilolo (asilimia 103) na Sumbawanga (asilimia 92)  huku zile zilizofanya vibaya kuwa ni Newala na Tandahimba (asilimia 15), Momba na Masasi (asilimia 13) na Nanyamba (asilimia 12)

Kwa kigezo cha pato ghafi, Jafo alisema halmashauri zinazongoza kwa wingi wa mapato kuwa ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma 9 (Sh bilioni 49.9), Ilala (Sh bilioni 44.8), Kinondoni(Sh bilioni 23.5) Temeke  Sh bilioni 20.6) na Jiji la Arusha (Sh bilioni 12.5) wakati halmashauri tano zilizofanya vibaya katika kundi hili ni Madaba(Sh milioni 293.7), Newala (Sh milioni 268.3) Kakonko (Sh milioni 238.6) Buhigwe (Sh milioni 177.3) na Momba(Sh milioni 170.4).

Aidha, katika kundi la mikoa kwa kigezo cha asilimia, Jafo alisema mikoa inayoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani ni Mkoa wa Iringa (asilimia 77), Geita (asilimia  73), Dar es salaam (asilimia  72), Dodoma na Songwe (asilimia  68) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Shinyanga (asilimia 46), Katavi (asilimia  43), Kigoma na Lindi (asilimia 42) na Mtwara (asilimia 26).


Kwa upande wa mikoa kwa kigezo cha pato ghafi, Jafo alitaja mikoa inayoongoza kuwa ni Dar es Salaam (Sh bilioni118.4) Dodoma (Sh bilioni 57.30), Mwanza (Sh bilioni 22.9) Arusha (Sh bilioni 22.8) na Mbeya (Sh bilioni 19.8) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Manyara (Sh bilioni 6.5) Lindi (Sh bilioni 6.1), Rukwa (Sh bilioni 5.8) Kigoma (Sh bilioni 4.5) na Katavi Sh bilioni 3.8).

Aidha, Jafo alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza katika kundi la halmashauri za majiji kwa asilimia kwa kukusanya asilimia 87 ya makisio huku jiji la Tanga likiwa la mwisho katikakundi hilo baada ya kukusanya asilimia 57 ya makisio.

Alisema Halmashauri ya Dodoma inaongeza kwa kigezo cha patoghafi ambapo imekusanya Sh bilioni 50 na halmashauri ya jiji la Tanga imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya Sh bilioni 8.7.

Aidha, Jafo alisema halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imeongoza kundi la halmashauri za Manispaa kwa kukusanya asilimia 92 ya makisio huku Lindi ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya asilimi 23 ya makisio.

Jafo alisema kwa upande wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeoongoza katika kundi la halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha mapato ghafi baada ya kukusanyw Sh bilioni 50 huku Tanga ikiwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 8.7.

Aidha, JAfo alisema halmashauri ya Mji wa Kondoa imeongoeza kundi la halmashauri za miji kwa kigezo cha asilimia ambapo wamekusanya kwa asilimia 92 ya makisio huku halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya asilimi 12 ya makisio.

“ Katika kigezo ya pato ghafi kwa halmashauri za mji, Geita inaongeza baada ya kukusanya Sh bilioni 5.9 na halmashauri ya mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho ikiwa imekusanya Shilingi milioni 293.9.


Kwa upande wa halmashauri za wilaya, Jafo alisema Mbozi inaongoza kwa kukusanya kwa asilimia 113 ya kamkisio nay a mwisho ni Masasi iliyokusanya asilimia 13 ya makisio wakati kwa upadne wa pato ghafi, Chalinze inaoongoza kwa kukusanya Sh bilioni 4.6 na ya mwisho katika kundi hili ni Momba iliyokusanya Sh milioni 170.4.

Aidha, Jafo aliwataka wakurugenzi ambao makusanyao yao hayajafika asilimia 50 kuaza kujitathimini huku asikisisitiza kuwapo taarifa za baadhi ya watumishi kuhujumu ukusanyaji wa mapato.

“ Mkurugenzi usikubali kurudishwa nyuma na watendaji wasio waamini, maana kuna baadhi ya maeneo watu wamekuwa wahatumii mifumo ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kieletroniki na wengine hawatumii kabisa,”

Aidha, Jafo ameendelea kusisitiza wakurugenzi kuhakikisha fedha za mapato ya ndani asilimia 40 au 60 kuelekezwe kwenye miradi ya maendeleo eneo husika sambamba na utoaji wa asilimia 10 za fedha za ndani kwa walemavu, vijana na wanawake na kusisitiza kuwa mwisho wa mwaka mambo hayao yatakuwa ni tathimini ya utendaji wa wakurugenzi hao.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.