• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Hali ya Ukusanyaji wa Mapato kwa Halmashauri Zote

Imewekwa tar.: April 23rd, 2020

Kwa mwaka wa fedha 2019/20 Halmashauri zilipanga kukusanya shilingi bilioni 765.48 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 Halmashauri zimekusanya Jumla ya Shilingi bilioni 527.31 ambayo ni asilimia 69 ya makisio ya mwaka.

Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya Halmashauri katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 umeonesha ongezeko la mapato yaliyokusanywa kutoka Shilingi Bilioni 449.82 kwa kipindi cha Julai, 2018 hadi Machi, 2019 na kufikia Shilingi bilioni 527.31 katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 ambalo ni ongezeko la  Shilingi bilioni 77 sawa na asilimia 17 .

Vile vile uchambuzi unaonesha kuwa katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 Halmashauri 58 zimekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 75 au zaidi kwa kulinganishwa na makisio kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Aidha, Halmashauri 96 zimekusanya asilimia 50 au zaidi lakini chini ya asilimia 75 na Halmashauri 31 zimekusanya chini ya asilimia 50 ya makisio ya mwaka.

Halmashauri hukusanya mapato mengi au kidogo kwenye vyanzo tofauti kulingana na hali halisi ya shughuli za kiuchumi za kila Halmashauri ikiwemo mavuno na mauzo ya mazao mbalimbali na katika kipindi hiki ushuru wa Huduma umekusanywa vizuri na umechangia asilimia 26 ya mapato yote katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato katika eneo hili unaonekana kuimarika.

Akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo  mapema leo amesema katika kipindi cha miezi tisa (Julai, 2019 – Machi, 2020), Halmashauri ya Mji wa Njombe imevunja rekodi kwa kukusanya mapato kwa asilimia 130 ya makisio ya mwaka 2019/2020 huku Halmashauri ya Wilaya ya Shinyangaikiwa ya mwisho kwa kukusanya  asilimia 30 tu ya makisio yake kwa kipindi cha miezi tisa.

Mhe. Jafo alifafanua kuwa halmashauri zote zilizokusanya zaidi ya asilimia 100 hadi Machi, 2020 na zile ambazo zimejitathmini na kuona upo uwezekano wa kuzidi asilimia 100 ya bajeti za mapato ya ndani ifikapo Juni, 2020 zinaelekezwa kufanya mapitio ya Bajeti kwa mujibu wa Kifunga cha 29 (1) cha Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 ili ziweze kuongeza Bajeti za mapato na matumizi ya fedha hizo.

“Halmashauri itakayoshindwa kufanya hivyo haitaweza kutumia fedha hizo kwa kuwa Bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 imekwisha idhinishwa na Bunge” alisisitiza Jafo.

Katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), Waziri Jafo ameeleza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi 43.14 na Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imekusanya mapato kidogo kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Milioni 343.70.  

Aidha Waziri Jafo amesema  mapato ya ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia asilimia kuwa Mkoa wa Njombe umefanya vizuri kwa kukusanya wastani wa asilimia 87 ya makisio ya Halmashauri za Mkoa huo huku Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Simiyu ambao umekusanya wastani wa asilimia 51 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo.

Katika kigezo cha mapato ya ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia wingi wa Mapato amesema Mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri kwa kukusanya kiasi cha Shilingi 126.77 huku Mkoa wa mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Rukwa ambao umekusanya Shilingi 6.34.

Jafo alibainisha ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa kuzingatia aina za Halmashauri kwa Kigezo cha Asilimia ya Makusanyo ukilinganisha na makisio kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya mapato kwa asilimia 78 ya makisio yake ya mwaka huku halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 55 ya makisio yake.

“Kwa upande wa Asilimia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeongoza kundi la Halmashauri za Manispaa kwa kukusanya  asilimia 100 ya makisio yake huku Manispaa ya Lindi ikiwa ya mwisho akwa kukusanya asilimia 49  kwa mwaka wa Fedha 2019/20” amesema Jafo.

Katika kipengele cha Halmashauri za Miji, Jafo amesema Halmashauri ya Mji wa Njombe imeongoza kwa kukusanya asilimia 130 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka na Mji wa Handeni imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 43 ya makisio yake kwa mwaka.

Aidha, kwa kundi la Halmashauri za Wilaya amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeongoza kwa kukusanya asilimia 126 ya makisio ya mapato ya ndani na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imekuwa ya mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya asilimia 30 ya makisio ya mapato yake ya ndani.

Waziri Jafo aliongeza kuwa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuzingatia wingi wa makusanyo ni Jiji la Dodoma ambalo limeongoza kundi la Majiji kwa kukusanya Shilingi bilioni 36.04 na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limekuwa la mwisho ambapo kwa kukusanya Shilingi bilioni 8.83.

Kwa upande wa Manispaa, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeongoza kwa kukusanya Shilingi bilioni 43.14 na Manispaa ya Kigoma Ujiji imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 1.20 amesisitiza Jafo.

Pia aliongeza kuwa  halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa wingi wa mapato kwa kukusanya Shilingi Bilioni 7.02 na Halmashauri ya Mji wa Mbulu imekuwa ya mwisho katika kundi kwa kukusanya Shilingi Milioni 671.78.

Na kwenye Halmashauri za Wilaya, Halmashauri  ya Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi ya Shilingi Bilioni 5.78 na  Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 343.70.

Halkadhalika Jafo alibainisha matumizi ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri kwa kipindi cha Julai 2019 – Machi 2020 kuwa  Halmashauri zimetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 329.53 ambayo ni asilimia 63 ya mapato halisi yaliyokusanywa na kati ya matumizi hayo, Shilingi Bilioni 186.75 zimetumika kwenye matumizi ya kawaida na Shilingi Bilioni 142.80 zimetumika kwenye matumizi ya maendeleo.

Amehitimisha  kuwa  Shilingi Bilioni 34.83 zimetumika kwenye miradi ya maendeleo ikiwa ni bakaa ya mapato ya ndani ya mwaka wa fedha 2018/19 ambayo ni asilimia 76.5 ya bakaa yote (Shilingi Bilioni 45.54), hivyo kufanya jumla ya matumizi ya miradi ya maendeleo kufikia Shilingi Bilioni 169.20.

Mwisho.



Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.