Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

DKT. MSONDE AONGOZA KIKAO KAZI KUTAFUTA UFUMBUZI WA CHANGAMOTO ZA WALIMU

Imewekwa tar.: June 21st, 2023

Na Mwandishi wetu – Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu, Dkt. Charles Msonde tarehe 21 Juni, 2023 ameongoza kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR – UTUMISHI), OR – TAMISEMI na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kilicholenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kiutumishi zinazowakabili walimu nchini.

Akifungua kikao hicho kilichofanyikia katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya TSC Makao Makuu Dodoma, Dkt. Msonde amesema kuwa pamoja na kuwa Serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha walimu wanapata maslahi yao, bado zipo changamoto kadhaa zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi ili walimu waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

“Serikali chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya juhudi kubwa kuwasaidia walimu kupata maslahi yao. Kwa mfano, sasa hivi walimu wanaendelea kupandishwa vyeo kwa wakati, madai ya mapunjo ya mishahara na madai ya fedha za likizo yameelipwa kwa kiasi kikubwa na bado yanaendelea kulipwa. Hata hivyo, pamoja na jitihada hizo bado tunaona zipo changamoto zinazowakabili walimu ambazo ni muhimu tuzitafutie ufumbuzi,” amesema Dkt. Msonde.

Amesema kuwa ofisi hizo tatu (OR – TAMISEMI, OR – UTUMISHI na TSC) zimeamua kukutana pamoja kupitia changamoto moja moja na kuona na kuweka mikakati ya namna ya kuzitatua kwa kuwa ndizo zenye dhamana ya kushughulikia masuala ya walimu nchini. 

“Waziri wetu, Mhe. Angellah Kairuki amukuwa akifuatilia kwa karibu sana masuala ya walimu. Ametoa namba yake ya simu ili mwalimu yeyote mwenye changamoto aweze kuwasiliana nae moja kwa moja. Na kila siku anapokea simu za malalamiko ya walimu wetu na anatuagiza sisi wasaidizi wake kutafuta ufumbuzi wa malalamiko hayo. Hivyo, leo tunapaswa kuhakikisha tukitoka hapa masuala ya walimu yamekaa vizuri,” amesema Naibu Katibu Mkuu huyo. 

Dkt. Msonde ameongeza kuwa ili kutatua changamoto hizo ni lazima kila mtendaji aliyepewa dhamana katika kusimamia walimu kuanzia ngazi ya shule, kata, halmashauri, mkoa na taifa kuhakikisha anakuwa msaada badala ya kuwa chanzo cha walimu kukosa haki zao. 

“Tunafahamu kuwa zipo changamoto za kiutumishi ambazo zimesababishwa na masuala ya kimfumo, lakini zipo ambazo zinasababishwa na uzembe wa watendaji wetu. Ni muhimu tuelewe kwamba ili kuinua elimu Tanzania ni lazima sisi watendaji tuliopewa dhamana tuhakikishe tunawajibika katika nafasi zetu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu,” amesema Dkt. Msonde.

Kwa Upande wake, Katibu wa TSC, Mwl. Paulina Nkwama amepongeza jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuweka mazingira bora ya elimu na walimu nchini ambapo alieleza baadhi ya jitihada hizo kuwa ni  walimu kuendelea kuajiriwa, kupandishwa vyeo, kubadilishiwa kazi waliojiendeleza kielimu, ujenzi wa nyumba za walimu na miundombinu mbalimbali ya shule.

“Tunampongeza Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye sekta yetu ya elimu, pia tunaipongeza OR - UTUMISHI kwa kazi nzuri waliyofanya kupandisha vyeo watumishi wa Umma wakiwemo walimu waliopandishwa vyeo wanathibitishwa na kulipwa mishahara kwa vyeo vyao vipya kwa wakati. OR – TAMISEMI tunawapongeza pia kwa namna wanavyofanya ufuatiliaji usiku na mchana kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira bora na wanatekeleza majukumu yao kikamilifu,” amepongeza Mwl. Nkwama. 

Nkwama ametaja baadhi ya changamoto zinazosababisha malalamiko kwa walimu kuwa ni baadhi yao kukaa kwenye daraja/cheo kimoja kwa muda mrefu, kucheleweshwa kubadilishiwa cheo baada ya kujiendeleza  kielimu, kutofautiana kwa vyeo kwa walimu wa kundi rika moja (walioanza kazi pamoja na wenye sifa sawa) pamoja na walimu wanaopanda vyeo pamoja kuidhinishiwa barua za kupanda vyeo kwa tarehe tofauti kwa sababu za kimfumo.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.