Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dkt. Dugange aitaka TSC kuendelea kutekeleza majukumu yake

Imewekwa tar.: October 18th, 2022

Na. Asila Twaha, OR - TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (AFYA) Dkt. Festo Dugange ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Tume hiyo.

Akifungua kikao cha wajumbe wa  Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oktoba 18, 2022 Jijini Dodoma, Dkt. Dugange amewataka  Watendaji wa Tume hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kusimamamia utumishi wa  walimu ambao ni zaidi  ya  asilimia 50 ya watumishi wa Umma nchini.

Dkt. Dugange Ameelezea na kutoa maelekezo kwa baadhi ya walimu kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa walimu kwa kufanya vitendo ambavyo havistahili katika utumishi ambapo jumla ya watumishi walimu 11,396 walichukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na walimu.

“ninaielekeza Tume kuendelea kuwachukulia hatua watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa walimu pale tu unapopatikana ushahidi usiotia shaka” amesisitiza Dkt. Dugange

Aidha, Dkt. Dugange ameitaka Tume hiyo kulifanyia kazi  suala la utoro kwa walimu 7,579 kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu kwa sababu inaweza kusababisha walimu kutowajibika na kupelekea hasara kwa wananchi wanaohudumiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi Bi. Paulina Mkwama ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuiamini Tume ya Utumishi wa Walimu pamoja na kushughulikia masuala ya kiutumishi wa walimu kwa kuajiri, kusajili walimu, kuwathibitisha kazini waliokidhi vigezo, kupandisha vyeo, kupandisha vyeo walimu waliojiendeleza, kushughulikia masuala ya kustaafu na kuelimisha walimu.

Aidha, ameiomba Serikali kuendelea kuangalia suala la Muundo wa Tume  ya Utumishi wa Walimu kwa kuwa muundo uliopo bado unaonyesha kuwa na uhitaji  wa Makatibu Wasaidizi wa Wilaya ambao bado hawajateuliwa.

Bi. Mkwama pia amesema kuwa tayari mapendekezo ya mabadiliko ya muundo wa Maendeleo ya Utumishi na mshahara kwa watumishi wa Tume ulishawasilishwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu ni kwa mujibu wa Kanuni ya 108 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 ikisomwa pamoja na  Kifungu cha 73 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Mwaka 2004.

Kikao hicho kina lengo la kuwaleta pamoja watumishi kwa kuwasilisha kero zao na kuzitafutia  ufumbuzi pamoja na kujadili majukumu ya Tume ya Utumishi wa Walimu chenye kauli mbiu ya "Kazi Iendelee"


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • FANYENI MSAWAZO SAHIHI WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA KATIKA HALMASHAURI ZENU – MHE. DKT. DUGANGE 

    June 10, 2025
  • MHANDISI SEFF AWATAKA MAKANDARASI MIRADI YA DHARURA (SERC)KUZINGATIA MASUALA YA USALAMA KAZINI NA UTUNZAJI MAZINGIRA.

    June 10, 2025
  • Vumbi Latimuka UMITASHUMTA Iringa: Dodoma, Songwe Zatingisha katika Mpira wa Mikono

    June 10, 2025
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025

    June 09, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.