Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Dar es Salaam Bingwa UMISSETA 2019

Imewekwa tar.: June 21st, 2019

Na Mathew Kwembe, Mtwara,

Mashindano ya 40 ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania UMISSETA yamefungwa rasmi jana katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara na Waziri wa elimu,sayansi,na teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako kwa mkoa wa Dar es salaam kutangazwa kuwa mshindi wa jumla wa UMISSETA 2019.

Katika mashindano ya mwaka huu jumla ya mikoa 28 ikiwemo miwili ya Unguja na pemba ilishiriki mashindano hayo.

Mkoa wa Dar es salaam ulishika nafasi ya kwanza baada ya washiriki wake kufanya vizuri kwenye michezo ya mpira wa kikapu wasichana ambapo walishika nafasi ya kwanza, wavu walishika nafasi ya pili wasichana na wavulana, soka walishika nafasi ya tatu wasichana.

Pia washiriki kutoka mkoa wa Dar es salaam walifanya vizuri katika mchezo wa mpira wa meza ambapo wasichana walishika nafasi ya kwanza, netiboli pia walishika nafasi ya kwanza, na riadha wavulana walishika nafasi ya pili.

 Nafasi ya pili ilichukuliwa na Morogoro,nafasi ya tatu ilienda  Mwanza, nafasi ya nne ilichukuliwa na Tabora na Mbeya ulishika nafasi ya tano.

Kabla ya kutoa hotuba yake, Mhe. Ndalichako na wageni waalikwa walipata fursa ya kushuhudia pambano kali la fainali soka wavulana kati ya Songwe na Ruvuma ambapo mshindi ilibidi apatikane kwa njia ya penati baada ya timu hizo kufungana goli 1-1.

Katika hatua ya penati Ruvuma ilifanikiwa kuchukua ubingwa  wa UMISSETA wavulana baada ya kuifunga timu ngumu ya Songwe kwa penati 10-9.

Mshindi wa tatu Soka wavulana ni Mwanza ambapo golikipa bora kwa upande wa soka wavulana ni Nice kahemele wa Ruvuma na kwa wasichana ni Safina Haule pia kutoka mkoa wa Ruvuma.

Mfungaji bora kwa upande wa soka wavulana ni Paul Nyerere wa Mwanza ambaye alifanikiwa kupata magoli 6 huku mfungaji bora kwa upande wa soka wasichana ni Aisha Hamisi wa Mwanza ambaye alifunga magoli 13.

Mchezaji bora wa mashindano ya UMISSETA 2019 ni John Chinguku kwa upande wa soka wavulana kutoka Ruvuma na kwa upande wa soka wasichana mchezaji bora ni Ester Daniel kutoka Mwanza.

Kwa upande wa wachezaji walioonyesha mchezo mzuri (fair play) kwa soka wavulana ni Jackson Simba wa Ruvuma na kwa soka wasichana ni Lucy Mwenda pia kutoka mkoa wa Ruvuma.

Mapema kabla  ya kugawa zawadi kwa washindi mbalimbali, Waziri Ndalichako alisema kuwa serikali inayathamini sana mashindano ya UMISSETA kama sehemu sahihi ya kupata wanamichezo wenye vipaji watakaoweza kutumika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Hivyo akataka wizara yake ihakikishe kuwa pindi wanapofanya ukaguzi shuleni wahakikishe pia somo la michezo linakuwemo.

Pia akataka kila shule inayosajiliwa ihakikishe kuwa inakuwa na viwanja vya michezo ili kuwawezesha watoto watakaosoma katika shule hizo kupata fursa ya kucheza michezo mbalimbali.

Waziri Ndalichako amesema kuwa michezo ni sehemu nuhimu sana kwa wanafunzi kwani inawajengea afya ya akili pindi wanaposhiriki michezo mbalimbali na hivyo kuwawezesha kusoma vizuri.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Mhe.Mwita Waitara amesema kuwa Ofisi yake itaendelea kuhakikisha kuwa michezo ya UMISSETA inafanyika ili kuwawezesha vijana wenye vipaji kuonyesha uwezo wao na hivyo kupata fursa ya kujiendeleza kimichezo.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.