Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Ajenda Upimaji maeneo ya Shule sasa basi-Serikali

Imewekwa tar.: December 21st, 2020

Serikali imesema ajenda kuu katika mwaka wa 2021 ni upimaji wa maeneo yote ya shule na kuyapatia hati miliki ili kuepusha migogoro na migongano ya mara kwa mara baina ya jamii na uongozi wa shule.

Akifungua Mkutano wa Mkuu wa 15 Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari nchini (TAHOSSA), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo amesema, amesiki kilio na malalamiko ya umoja huo juu ya maeneo mengi ya Viwanja vya shule kutopimwa na kufanya wananchi kuvamia bila utaratibu, hivyo ajenda kuu katika mwaka wa 2021 ni kuhakikisha maeneo yote yanapimwa na kumilikishwa kwa taasisi hizo za serikali.

“Nawaagiza Wakurugenzi wote nchini, hili suala la upimaji sasa lifikie mwisho, leo ni tarehe 21 Desemba, 2020 ifikapo mwakani tarehe kama ya leo suala hili tusingependa kulisikia tena, kama ni wataalam wa ardhi wapo kila Halmashauri hivyo basi Wakurugenzi wawasimamie ili kukamilisha zoezi hili muhimu” amesema Mhe. Jafo

Katika hatua nyingine Mhe. Jafo amesema, Serikali inayo nia ya dhati yakuhakikisha Watoto wa kitanzania wanapata elimu bora kwakuwaboreshea mazingira bora ya kujifunza na kusomea, kwani kila mwezi fedha zinazo tolewa  kwaajili ya elimu bila malipo zimefikia bilioni 24, ametaja kuwa hayo ni mafanikia makubwa, huku akisema serikali pia imetenga  bilioni 68 kwenye bajeti katika mwaka wa fedha   2020/21, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 2,088 kwa shule za Msingi na shilingi 103,984,000 kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba vya maabara vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi.

Waziri Jafo amewahakikishiwa wajumbe hao kuwa, ifikapo Juni, 2021, shule zote Kongwe 89 zinazokarabatiwa zitakuwa zimekamilika na kuonekana mpya na kwamba, hadi sasa kuna jumla ya shule 73 zilizokwisha kukamilika na ukarabati unaendelea kwenye shule 13 kati ya 16 ambazo nazo zitakarabatiwa kulingana na ratiba ya kazi hiyo. “Lengo letu ni kuimarisha mazingira ya kufundisha na kujifunzia amesisitiza Waziri Jafo.

Akitoa salaam za Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli alisema, Serikali imefanya mapinduzi Makubwa katika sekta ya elimu ikiwepo matumizi ya TEHAMA.

“Kwa sasa unaweza kukaa Ofini kwako na ukapata idadi ya kamili ya wanafunzi kupitia mfumo wa (School Information System-SIS) kwakuwa ni mfumo unao kusanya takwimu za kila siku na kuzichakata kwa ajili ya matumizi”.  Amesema Mweli na kuongeza kuwa ili Shule iweze kupata Fedha  PREM ni lazima uwekaji na utunzwaji wa takwimu kupitia mfumo huo ziwe madhubuti.

Awali akitoa salamu za Umoja huo Rais wa TAHOSSA Taifa, Frank Yesaya alimkumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa ushindi wa kishindo wa asilimia 84 huku akiahidi kwa niaba ya Umoja huo, kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali zakumkomboa mtoto wa kitanzania kwa kumpatia elimu iliyo bora.

“Mhe. Waziri tukuhakikishie kwamba, Umoja huu upo tayari kushikiana na Serikali wkati wote na salam hizi tunaomba zimfikie Mhe. Rais, mwambie tunaunga mkono juhudi za Serikali chini ya uongozi wake, kwakuwa ni Rais mwenye maono na moyo wa kizalendo kwa nchi yake” amesema Rais wa TAHOSSA.

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania, ambao ni Mkutano wa 15, umefanyika jijini Dodoma ukiwa na kauli mbiu,Elimu bora kwa uimarishaji wa uchumi wa kati


Na Atley Kuni-TAMISEMI, Dodoma

Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • MAHUSIANO MAZURI  NI NGUZO MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU-MHE.SAGINI

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.