• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Agizo kwa Halmashauri ya Wilaya Masasi baada ya kusuasua kwa ujenzi wa madarasa

Imewekwa tar.: November 28th, 2021

Na Fred Kibano, Masasi Mtwara

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Festo Dugange ameiagiza Halmashauri ya Wilaya Masasi kuharakisha ujenzi wa madarasa katika halmashauri hiyo unakamilika kwa wakati.

Akiongea na watendaji wa halmashauri za Masasi Mji, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mbele ya Wenyeviti wa Halmashauri hizo na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Claudia Mkya, Dkt. Dugange hapo jana amesema hatakuwa tayari kuangushwa na Watendaji, badala yake wafanye kazi usiku na mchana na kuhakikisha miradi ya ujenzi wa madarasa yote inakamilika ifikapo tarehe 15 Desemba, 2021.

“halmashauri ya wilaya ya Masasi bado mnachechemea  kwenye ujenzi wa madarasa kwa zaidi ya asilimia 60 hadi 70, bado mpo katika hatua ya msingi sasa hiyo siyo dalili njema, Mkurugenzi na Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Masasi lazima mkajipange, muhakikishe miradi inakamilika kwa wakati, hayo ni maelekezo na hamtakiwi kujitetea na mimi sipo tayari kuangushwa” alisema Dkt. Dugange

Dkt. Dugange amewataka kukamilisha miradi hiyo kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha na siyo kujenga kwa haraka bila kufikia viwango vinavyokubalika. Aidha, amesema fedha zilizotolewa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya madarasa imewekwa pamoja na madawati na viti na hivyo ujenzi wa madarasa uendane sambamba na manunuzi ya samani za darasani.

Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mheshimiwa Claudia Mkya amekiri kuwa halmashauri hiyo imekuwa na kasi ndogo kwenye ujenzi wa madarasa kutokana na changamoto ya upatikanaji wa maji na kuchelewa kupata saruji iliyoagizwa kutoka kiwanda cha Dangote na sasa changamoto hizo zimetatuliwa, hivyo basi amepokea maelekezo na atasimamia kwa kuhakikisha wanajenga usiku na mchana ili kukamilisha miradi katika muda uliopangwa.

Awali akitoa taarifa kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bw. Apoo Tindwa amesema halmashauri yake ilipokea fedha za ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19 kiasi cha shilingi Bilioni moja na milioni 960 kwa ajili ya kujenga madarasa 84 ya sekondari na madarasa 14 ya shule za msingi na kwamba yapo katika hatua mbalimbali.

“madarasa 26 yapo kwenye hatua ya ujenzi wa maboma, madarasa 4 ujenzi upo kwenye hatua ya linta na madarasa 68 ujenzi upo kwenye hatua ya msingi”

Amezitaja changamoto zilizosababisha kuchelewa kwa ujenzi wa madarasa kuwa ni pamoja na upatikanaji wa maji, kutokupatikana kwa tofali za kununua kwa bei isiyozidi shilingi 1,500 kwa tofali moja na ucheleweshwaji wa saruji kutoka kiwandani.

Mapema mwaka huu Serikali ilipeleka fedha kwenye halmashauri zote kwenye nchi nzima ili kuhakikisha inapofika mwaka 2022 januari wanafunzi wote waliofaulu na kupangiwa shule kuanza kidato cha kwanza wanaanza masomo kwa pamoja bila kuwa na chaguo la pili na la tatu.


Matangazo

  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BASHUNGWA AWAAGIZA VIONGOZI WA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTANGAZA MIRADI YA MAENDELEO.

    July 02, 2022
  • Mameya, Wenyeviti wa Halmashuri watoa kongole kwa Rais Samia kuibadili Dodoma

    June 30, 2022
  • MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO- PROF. SHEMDOE

    June 30, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAFUNDA MAMEYA, WENYEVITI WA HALMASHAURI

    June 27, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.