Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Afisa Elimu Chamwino asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Imewekwa tar.: July 17th, 2019

Na Mathew Kwembe, Chemba

Aliyekuwa  Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Chemba  iliyopo mkoani Dodoma Mwalimu David Mwamalasa ambaye hivi sasa amehamishiwa wilaya ya Chamwino amesimamishwa kazi na serikali kwa muda wa wiki mbili ili kupisha uchunguzi dhidi yake wa matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 259 ambazo zililetwa na serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili mradi wa P4R kwenye Shule za sekondari za Mondo na Soya  zilizopo wilayani Chemba, katika mkoa wa Dodoma.

Agizo la kumsimamisha Afisa Elimu huyo limetolewa jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Mwita Mwikwabe Waitara (MB) mara baada ya kufanyika mkutano wa hadhara shuleni hapo ambao uliwahusisha wanafunzi, walimu na wakazi wa kijiji cha Mondo, katika wilaya ya Chemba.

Sambamba na kusimamishwa kwa Afisa elimu huyo ambaye alihamishiwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Mhe.Waitara amemwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamuhanga kuunda timu ya uchunguzi itakayokwenda shuleni hapo ili kuchunguza tuhuma hizo.

“Timu ije hapa ndani ya wiki mbili tupate fedha zilizoelekezwa kwa nini zimetumika kinyume na maelekezo, hayo ndiyo maelekezo yangu,” amesema Mhe.Waitara na kuongeza:

“Jambo lingine ambalo nimemwelekeza Katibu Mkuu, ni la kuhakikisha kuwa kuanzia sasa mtumishi anapofanya makosa eneo moja asihamishwe kwenda eneo linguine kwa nafasi yake ileile na kwa kweli hatupendelei kama viongozi, hata Mhe.Rais hataki, mtendaji yoyote ambaye atakuwa TAMISEMI amefanya makosa katika shule ya Mondo, natolea mfano kwa nafasi hiyo hiyo, hatuwezi tukawa tunasambaza uozo, kama mtu amekosa achukuliwe hatua, kama ni kuwa demoted (kushushwa cheo) ama kufukuzwa kazi ili na wengine wajifunze wasifanye makosa yale yale.”

Naibu Waziri amesema serikali haiwezi kuendelea kuwa na mtindo wa aina hiyo ambapo unafanya makosa sehemu A unahamishiwa sehemu B, badala yake akataka mhusika anapokutwa na makosa awajibishwe kwa kuondolewa nafasi yake ili apishe watumishi wengine ili wachukue nafasi hiyo.

Pia Mhe.Waitara alitumia mkutano huo kueleza bayana kuwa serikali haina mpango wa kufuta ngazi za kidato cha tano na sita katika shule hiyo na badala yake itaelekeza nguvu zake katika kuiboresha shule hiyo kwa kuiongezea miundombinu ya shule na walimu shule hiyo ili iweze kufanya vizuri katika mitihani itakayofanyika siku za usoni.

Amesema kuwa kamwe hatarajii kuona shule hiyo ikiondoa michepuo ya kidato cha tano kwani shule hiyo ina michepuo mitatu ya sayansi shuleni hapo na ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa miundombinu hiyo inaboreshwa kadri siku zinavyosonga mbele.

Awali Mratibu wa Mradi wa P4R (Lipa kwa matokeo) kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Mary Machaku alimweleza Naibu Waziri kuwa shule ya Mondo ilikuwa ni miongoni mwa shule 86 ambazo zilikuwa kwenye mpango wa serikali wa kuanzisha kidato cha tano.

Amesema kiasi cha shilingi milioni 259 zilizoletwa katika shule za Mondo na Soya wilayani Chemba zilileletwa na maelekezo mahsusi ambapo Afisa Elimu Sekondari wa wilaya pamoja na Mkuu wa shule walipaswa kuwatolea nakala wajumbe wa Bodi ya shule ili watekeleze maagizo ya namna ya kuzitumia fedha hizo na siyo kubadilisha matumizi kwa kuziachia bodi za shule  kutengua maelekezo ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Amesema kwa mujibu wa maelekezo ya TAMISEMI, fedha hizo zilipaswa kujenga mabweni mawili yenye kubeba wanafunzi 80 wa kidato cha tano kwa kila bweni, pia ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa kwa gharama ya shilingi milioni 20 kwa chumba kimoja cha darasa, hivyo jumla milioni 80 kwa vyumba vinne.

“Pia tulileta milioni 11 na laki moja kwa ajili ya ujenzi wa matundu 11 ya vyoo, sambamba na hilo tuliwaletea shilingi milioni 18 kwa ajili ya ukarabati wa maabara moja ambayo itakapokamilika iwe na mifumo ya maji, umeme na samani zake za ndani, ambapo total yake inaleta shilingi milioni 259,” amesema.

Katika utetezi wake, afisa elimu Mwamalasa alisema kuwa  maelekezo yote ya TAMISEMI kuhusu matumizi ya fedha hizo yalitekelezwa isipokuwa kwenye eneo la ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa ambapo bodi ya shule iliona afadhali ikarabati vyumba vitatu vya madarasa katika shule hiyo ambavyo vilikuwa vimeharibika kabisa, na vyumba vitatu vingine ambavyo vilirudiwa kufanyiwa kazi.

Mwamalasa amesema kuwa fedha hizo pia zilitumika kununulia vitanda 160, ukarabati wa ukumbi wa kulia chakula, na kuweka uzio upande wa mbele na nyuma kwa ajili ya kuimarisha usalama wa wanafunzi wa kike katika shule hiyo.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Chemba ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Elimu kutoka TAMISEMI Bibi Odilia Mushi.

 

Matangazo

  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • MAPEPELE AWANOA MAAFISA HABARI WA TAMISEMI, AWATAKA WAWE WAZALENDO 

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.