• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Zingatieni Sheria, Kanuni na Miongozo Kuepuka Migogoro – Mhe. Makilagi

Imewekwa tar.: May 4th, 2023

Na Fred Kibano, Mwanza

Serikali imewaasa Wahandisi na Maafisa Manunuzi waliopata mafunzo ya usimamizi wa manunuzi ya vifaa na ujenzi wa shule za Mradi wa BOOST kufuata sheria ili kufikia malengo na kuepuka migogoro.

Akifunga mafunzo hayo ya siku mbili Jijini Mwanza hivi leo tarehe 04.05.2023, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Amina Makilagi ambaye alitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Adam Ally Malima amewaasa Maafisa hao kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kutekeleza miradi yenye tija, kwa wakati na kuepuka migogoro.


“Ofisi ya Rais TAMISEMI inaamini weledi mlio nao katika kusimamia miradi, naomba niwakumbushe kutekeleza uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ili kupata thamani ya fedha na kuepuka hoja za ukaguzi. Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma, Sheria za Manunuzi, Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, na Sheria ya Bajeti” amesema Mheshimiwa Makilagi.

Aidha, amewaasa kuimarishaji ushirikiano ngazi ya Halmashauri ili Kila mmoja atimize majukumu yake kwa kushirikiana na wenzake na pia utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu kwa wakati na kwa ubora lakini pia kuepuka migogoro ambayo huchangia kuchelewesha utekelezaji wa miradi.

Pia Mhe. Makilagi amewaasa Maafisa hao kuendesha mafunzo waliyoyapata kwa Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Shule zitakazotekeleza miradi ya ujenzi kupitia mradi wa BOOST, kutobadilisha maeneo/shule zitakazopangiwa ujenzi/ukarabati wa miundombinu kwani Ofisi ya Rais TAMISEMI ilishafanya tathmini ya ujenzi wa shule na ukarabati wa miundombinu chakavu hivyo kusiwepo na ubadilishaji wa maeneo.


Amesema Serikali imeamua kuendesha mafunzo hayo ili kuwezesha kuandaa taratibu sahihi za  ujenzi wa shule mpya na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule zenye upungufu wa miundombinu hiyo ili kuwawezesha kupata uelewa wa pamoja kuhusu masuala yote ya kuzingatia kabla na wakati wa ujenzi wa miundombinu ya shule lengo kuu likiwa kutimiza masharti na vigezo vyote vilivyowekwa. 


Kwa upande wake Bwana joel Mhoja Mratibu Msaidizi Mradi wa BOOST amemshukuru Mheshimiwa Amina Makilagi na kuahidi kuyatekeleza yote yaliyofundishwa ikiwa ni pamoja na usimamizi wa mchakato mzima wa Mradi wa BOOST.


Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya shilingi Bilioni 230 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu kwenye shule 1,338 za msingi zilizopo katika Mikoa na Halmashauri zote nchini ili kujenga shule mpya 302 zenye vyumba 3,276 vya madarasa, madarasa 604 ya Awali ya mfano, majengo ya utawala 302 na matundu ya vyoo 6,160


Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo Maafisa Manunuzi na Wahandisi yanahusu juu ya usalama wa mazingira, ramani za mpangilio wa majengo na mapitio yake, tafsiri rasmi ya taratibu za manunuzi, utunzaji wa kumbukumbu za manunuzi na utambulisho wa DLI na vigezo vya uhakiki kwenye Mradi wa BOOST.


Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.