Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Zaidi ya watu Milioni 16 wajiandikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2019

Imewekwa tar.: October 16th, 2019

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amesema hadi sasa uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa umefikia watu milioni 16.9  kati ya malengo  yaliyowekwa ya watu milioni 22. 9 sawa na asilimia 74.

Mhe Jafo amesema hayo leo wakati wa kutoa tathimini ya uandikishaji wa Wapiga kura katika Orodha ya Daftari la wapiga kura katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika katika Ofisi za TAMISEMI Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amesema kumekuwa na hamasa kubwa kwenye uandikishaji baada ya viongozi mbalimbali hususani Wakuu wa Mikoa na wilaya kuingia mitaani kuhamasisha wananchi.

Mhe Jafo anafafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kuandikisha wapigakura kwa asilimia 89. Wakati hali bado tete kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo mpaka jana  ikiwa ni siku ya kwanza tangu kuongezwa muda wa kuandikisha imeadikisha kwa asilimia 37 tu.

Amesema mpaka sasa wapiga kura 16,906,545  wameandikishwa ikiwa ni sawa na asilimia 74 huku Dar es Salaam iliyoandikisha kwa asilimia 89 ikiwa kinara ikifuatiwa na Pwani iliyoandikisha kwa asilimia 86, Tanga kwa asilimia 81, Mtwara kwa asilimia 80 na Lindi kwa asilimia 77.

Mhe. Jafo anaendelea kusema kuwa kwa upande wa Mikoa hakuna Mkoa ulioandikisha chini ya asilimia 50, hata hivyo Mkoa ulioandikisha chini zaidi ni Kigoma iliyoandikisha kwa asilimia 57, Kilimanjaro kwa asilimia 58, Arusha na Shinyanga kila mmoja ukiandikisha kwa asilimia 66.

Akifafanua kuhusu Halmashauri zilizofanya vibaya amesema hali ni mbaya kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambayo imeanikisha kwa asilimia 37 na kufuatiwa na Halmashauri ya Moshi na Korogwe ambazo  kila mmoja

imeandikisha kwa asilimia 51.

Awali akitoa tathimini ya uandikishaji wa siku saba za mwanzo zilizoishia Oktoba 14,  Mhe. Jafo amebainisha  wapigakura walioandikishwa walikuwa milioni 15.5 ambao ni sawa na asilimia 68 ya lengo la kuandikisha wapigakura milioni 22.9 huku Mkoa wa Pwani uliongoza kwa kuandikisha kwa wastani wa asilimia 80, ikifuatiwa na Dar es Salaam kwa asilimia 77, Tanga ikiandikisha kwa asilimi 76, Mtwara na Lindi kila mmoja kwa asilimia 75.

Pia Kilimanajro ilishika mkia kwa kuandikisha wastani wa asilimia 48, ikifuatiwa na Kigoma kwa asilimia 53 Arusha kwa asilimia 59.

Wakati huohuo Mhe. Jafo amesema anawashangaa  wanasiasa wanaobeza kuwa uchaguzi na uandikishaji wa mwaka huu ni wa kusuasua na kuwataka kuacha upotoshaji na kujikita kwenye takwimu za ukweli ambapo uandikishaji ulikuwa mkubwa ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2014.

Amefafanua kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, Watanzania zaidi ya milioni 11.49 (11,491,661) ikiwa ni asilimia 62 ya makadilio ya kuandikisha watu 18,587,742 walijiandikisha katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka 2014

Aidha, Mhe.Jafo amesisitiza kuwa watumishi wa umma hawalazimishwi kujiandikisha na kuwa hakuna hatua au adhabu yeyote  itakachochukuliwa kwa asiyejiandikisha na kuwa kinachofanyika ni kuhamasisha ili kuhakikisha demokrasia inachukua mkondo wake.

“ Kanuni za uchaguzi ziko wazi, hakuna mtu analazimishwa ila kinachotakiwa kufanyika ni watu kuhamasishwa. Tumeona sehemu zingine kuna maandamano ya pikipiki au magari ya kuhamasisha na hili jambo jema kwa nchi yetu, kujiandikisha kunampa fursa mtu ya kwenda kuchagua kiongozi, ukikosa fursa hiyo unaweza baadaye kulalamika umechangua kiongozi ambaye haleti maendeleo” Amesisitiza Mhe. Jafo

Akizungumzia kuhusu “clip za  video” zinazotembea kuwa asiojiandikisha atakosa fursa zingine za maendeleo,  amesisitiza kuwa kanuni  ziko wazi, suala la kujiandikisha na kupiga kura ni hiyari na  mambo haya siyo maelekezo ya Ofisi ya TAMISEMI, watu wanatakiwa kuambiwa faida za kujiandikisha na kupiga kura kwa mustakabali wa maendeleo  ya Taifa.

Hata hivyo, Mhe. Jafo amefafanua kuhusu taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya  watumishi wa Jiji la Dodoma kulazimishwa kujiandikisha  na kusema kuwa lengo lilikuwa ni kuwahamaisha watumishi kwasababu wao wanafanya kazi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo ni vyema wakawa mstari wa mbele kujiandikisha ili kuwahamasisha wengine kujiandikisha.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.