Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

WAZIRI UMMY: TAMISEMI ni kubwa sio ngumu

Imewekwa tar.: April 1st, 2021

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watendaji wa TAMISEMI kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikano, ubunifu, uzalendo na uadilifu ili kurahisisha  mtendaji kazi.

Akiongea  leo na Menejimenti  ya ofisi hiyo katika hafla fupi ya ukaribisho  Mtumba,  Jijini Dodoma Waziri Ummy amesema kuwa atahakikisha anafanya kazi kwa ushirikiano, umoja na kujituma ili kuhakikisha TAMISEMI inakidhi matarajio ya Rais na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan

“ Baadhi ya watu wanasema TAMISEMI ni ngumu,  mimi nasema TAMISEMI sio ngumu, kama TAMISEMI ni ngumu maana yake mmeshindwa kunisaidia mimi na Manaibu Waziri kutekeleza wajibu wetu, ila tunakubali ni kubwa lakini hakuna kigumu kama kuna utendaji kazi wa pamoja” amesisitiza Waziri Ummy

Anaendelea kufafanua kuwa kinachohitajika ni  kufanya kazi kwa umakini, utekelezaji wa majukumu kwa wakati, na kuhakikisha tunaendeleza pale alipoachia aliyekuwa Waziri wa Nchi – TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo.

Aidha, Waziri Ummy amesema vipaumbele atakavyoanza navyo kuvifanyia kazi ni kupitia hoja zilizoibuliwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hasa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopata hati chafu nane na zenye mashaka 53.

Amesema vingine ni kuimarisha usimamizi wa makusanyo ya ndani na matumizi katika mamlaka hizo, ushirikiano na ubunifu, usimamizi wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo na urejeshaji wa fedha za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Kadhalika, amesisitiza kuzitambua changamoto zilizopo sekta ya afya, elimu na miundombinu ili kuzipatia ufumbuzi.

“Mmemsikia Spika(Job Ndugai) hivi Mkurugenzi unakuwaje na amani wakati watoto wanakaa chini, kitu kama madawati  hivi Mkurugenzi anajisikiaje watoto kukaa chini, hivi sisi TAMISEMI tunashindwa kuja na mkakati wa kuondoa tatizo la watoto kukaa chini, hivi TAMISEMI tunashindwa kuhakikisha madarasa yanajengwa ili watoto wasirundike kwenye madarasa wa kuwa na madawati na madarasa, nyumba za walimu hiki ni kipaumbele changu,”amesema.

Kuhusu utoaji wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Waziri Ummy ametaka kujua fedha zilizorejeshwa na kuzitaka Halmashauri kueleza mrejesho ili fedha zitolewe zaidi.

“Sitaki kusema mimi ni hodari bali ni hodari wa kushirikiana na wenzangu naamini tutakwenda vizuri,na kubwa lazima tuonyeshe matokeo hasa kwenye ukusanyaji wa mapato,”amesema.

Aidha amewaagiza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA), kushughulikia hoja zilizobainishwa na wabunge huku akisisitiza suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.