Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Mkuu aagiza kutenga Bajeti ya Matengenezo ya Magari 184 ya Maafisa Elimu

Imewekwa tar.: May 21st, 2021

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmsahauri zote nchini kuhakikisha wanapanga bajeti ya kufanyia matengenezo magari ya Halmashauri ili yaweze kudumu kwa muda mrefu

Akizungumza na Maafisa Elimu wa Halmashauri ya zote 184 Nchini wakati wa Uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa  Magari  kwa maafisa  hao yaliyonunuliwa kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo mapema leo katika Viwanja vya Shule ya Sekondari  ya Kibasila  Mkoani Dar-es-salaam amesema

‘Kuna baadhi ya Halmashauri hazitengi bajeti  kwa ajili ya matengenezo ya magari yao , na kusababisha  magari hayo kuharibika mapema na kuwekwa Gereji bila matengenezo  ya Halmashauri zao

“Maafisa elimu wa Wilaya Mkikabidhiwa magari haya leo na tukalikuta gari limekaa na halifanyi kazi kwa kukosa matengenezo lazima Wakurugenzi wa Halmashauri watawajibishwa “ amesisitiza Majaliwa

Amesema kila Halmashauri lazima iweke mpango wa matengenezo wa magari hayo ili ziweze kufanyakazi  kwa muda mrefu  na kuweza kufamnya kazi iliyopangiwa ya kuhakikisha inafanya ufutiliaji wa elimu katika shule za msingi nchini.

Amefafanua kuwa magari hayo yatumike kwa ajili ya ufuatiliaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Halmashauri na kuhakikisha yanafuatilia ufundishaji na ujifunzaji wa elimu katika Wilaya ili malengo yaweze kufikika na kukamilika kwa wakati

Amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya  kuwachukulia hatua  maafisa Elimu wote ambao watayatumia magari hayo kinyume na kazi iliyopangiwa ya ufuatiliaji wa masuala ya Elimu katika Halmashauri  kwa kuwa watakuwa wameenda kinyume na matakwa ya Serikali

Hata hivyo, amewaagiza maafisa elimu wote nchini kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi kwa kuwa ndio msingi wa mafanikio katika maeneo yao kwa kuwa kiwango cha mafanikio ya elimu kilichofikiwa bado kinahitaji nguvu zaidi ili tuweze kufik mbali zaidi.

‘Tunatambua changamoto zinazoendelea katika Halmashauri zenu na Serikali inatambua umuhimu wa elimu niwatake muendelee kufanyakazi kwa weledi na uaminifu ili kuongeza ufaulu na Serikali itaendele kutatua changamoto zenu’amesisistiza Majaliwa

Amewataka kuhakikisha wanawatia moyo waalimu katika kutekeleza majukumu yao , watembeleeni, wasikilizeni na  wahudumieni kwa kufuata sheria na taratibu za  utumishi wa umma  na imarisheni mahusiano katika utendaji kazi wa kila siku ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuongezaufaulu kwa wanafunzi.

Aidha ametaka Maafisa Elimu Nchini kuwatumia Madiwani  katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto na kuhakkisha wazazi wanawajibika katika suala zima la kutimiza majukumu yake katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu  amesema   magari hayo  yamenunuliwa na Serikali  kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo kwa  gharama ya shilingi  bilioni 16.4.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.