Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

WAZIRI KAIRUKI AWASILISHA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 9 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Imewekwa tar.: April 14th, 2023

Na. Fred Kibano – OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 leo Ijumaa tarehe 14 Aprili, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri Kairuki ameomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 9,144,021,699,000 (Trilioni Tisa) ambazo ni matumizi ya kawaida ya Ofisi, mishahara ya watumishi, Mikoa, Halmashauri, Tume ya Utumishi wa Walimu na Miradi ya Maendeleo.

Waziri Kairuki ametoa maelezo ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuwa katika eneo la Usimamizi na Uendeshaji wa Elimumsingi jumla ya wanafunzi wa Elimu ya Awali waliandikishwa 1,411,810, sawa na asilimia 103.52 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 1,363,834 ukilinganisha na mwaka 2023 ambapo wanafunzi 1,500,227 wameandikishwa ikiwa ni asilimia 109.37 ya lengo la kuandikisha wanafunzi 1,371,690 wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,411 ikiwa 1,211 wasichana na wavulana 1,200. 

Waziri Kairuki amesema mafanikio ya kuandikisha wanafunzi wengi kwa ongezeko la wanafunzi 88,417 sawa na asilimia 3.38 ikilinganishwa na wanafunzi walioandikishwa mwaka wa 2022 yametokana uhamasishaji wa Jamii, ujenzi  wa vituo shikizi na kuendelea kutoa ElimuMsingi Bila Ada.

Kuhusu upungufu wa walimu, Waziri Kairuki amesema hadi Februari, 2023 mahitaji ya walimu katika Shule za Msingi yalikuwa 362,189 kwa kutumia uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 45 ambapo walimu waliopo ni 175,864 na upungufu ni 186,325 sawa na asimilia 51.44 ya mahitaji.

Aidha, amesema mahitaji ya walimu kwa Shule za Sekondari ni 174,632 ambapo waliopo ni 84,700 na upungufu ni walimu 89,932 sawa na asilimia 51.5 lakini pia mahitaji ya walimu kwa shule za Sekondari yanatokana na masomo yanayofundishwa.

Kuhusu utekelezaji wa Afya ya Msingi Waziri Kairuki amesema, katika Mwaka wa Fedha wa 2022/23 ziliidhinishwa Shilingi Bilioni 143.15 kupitia ruzuku ya Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Afya ya Msingi ambapo hadi Februari, 2023 Shilingi Bilioni 124.10 zimepokelewa sawa na asilimia 86.69 ya fedha iliyoidhinishwa.

 Waziri Kairuki amesema Shilingi Bilioni 69.95 ziliidhinishwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi Bilioni 15.15 ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa  kwa zahanati 300, Shilingi Bilioni 47.70 kwa Vituo vya Afya 159 na Shilingi Bilioni 7.10 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba vya afya ya kinywa, meno na macho kwa hospitali za Halmashauri 71 zilizokamilika na hadi kufikia Februari, 2023 jumla ya Shilingi Bilioni 54.55 zilikuwa zimepokelewa, sawa na asilimia 77.98.

Hadi Februari, 2023 Halmashauri zimekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 625.31 sawa na asilimia 62 ya makisio kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/23 ikiwa ni ongezeko la Shilingi Bilioni 9.70 sawa na asilimia 1.57 ikilinganishwa na makusanyo ya Shilingi Bilioni 615.61 yaliyokusanywa kwa kipindi kama hiki katika Mwaka wa Fedha wa 2021/22.

“katika kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imefanyia kazi changamoto zilizokuwepo katika mfumo wa mapato wa Local Government Revenue Collection Information System (LGRCIS) kwa kusanifu na kujenga mfumo mpya wa TAUSI ambao umeanza kutumika katika Mwaka wa Fedha wa 2022/23” amesema Kairuki.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.