Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waziri Jafo awataka wahitimu wote kuwa wabunifu katika kulitumikia taifa

Imewekwa tar.: December 18th, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Seleman Jafo ametoa wito kwa wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kujiandaa kufanyakazi kwa bidii na kuleta mabadiliko katika jamii pale wanapopatiwa dhamana ya kulitumikia Taifa

Waziri Jafo ametoa wito huo leo katika mahafali ya 34 katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampusi kuu ya Dodoma na kuwataka wahitimu hao kujiaanda kisaikolojia kwenda kulitumikia taifa linalokuwa kwa kasi kimaendeleo.

“Nendeni mkafanye kazi, Nendeni mkawajibike, mkawe mfano kwa jamii ambayo mtaitumikia na kuleta mabadiliko, msijikweze kwa ajili ya elimu mliyonayo bali mkawasaidie wananchi katika kuleta maendeleo, hii ndio ikawe nguzo yenu,” amesisitiza Waziri Jafo

Amesema kuwa chuo cha Mipango kimewajenga katika misingi ya umahiri ambao unawasaidia wahitimu katika Soko la ajira na kukuza uchumi wa nchi, hivyo fanyeni kazi kwa umakini na ubunifu mkubwa pale unapopatiwa nafasi katika Sekta binafsi au Serikalini ili kulinda heshima ya chuo hicho.

Amewataka Wahitimu kushirikiana na jamii katika masuala ya maendeleo kwa kuwa waaminifu ili jamii ijivunie kuwa na wasomi wabobezi ambao wataleta chachu ya maendeleo katika maeneo yao.

Waziri Jafo ameendelea kufafanua kuwa wahitimu watakaopata nafasi ya kulitumikia Taifa wahakikishe wanafanyakazi kwa weledi na uaminifu mkubwa ili kuacha alama na kumbukumbu kwenye maeneo yao ya kazi.

Aidha, amewataka wahitimu hao kuhakikisha wanatunza amani ya nchi ili Taifa liweze kufanya shughuli zake za kimaendeleo kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha Mipango ya maendeleo vijijini Prof. Hozen Mayaya amesema katika mwaka wa masomo 2018/2019 kwa kampasi kuu pekee kumekuwa na ongezeko la udahili wa wanafunzi wapya kutoka wanafunzi 4,317  mwaka 2019/2020 hadi wanafunzi 5,856 ikiwa ni ongezeko asilimia 26.

Ameeleza kuwa wahitimu waliomaliza masomo yao mwaka huu ni wanafunzi 4072 ambapo kati ya hao wanaume  ni 1.756 na wanawake  2, 316 ambapo ni ongezeko la  asilimia 27 ukilinganisha na wahitimu wa mwaka  2018.

Kwa kuongezea Prof. Mayaya amesema kuwa chuo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kimeendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha hali maisha ya wananchi ikiwa ni pamoja mradi wa kuboresha ustahimilivu wa jamii za wafugaji na wakulima wa Serengeti kwa ajili ya kupunguza migogoro ya Rasilimali za kiikolojia na nyingine zinazofanana na hizo(2019-2023).

“Miradi mingine ni mradi wa kuwajengea uwezo watumishi wa mamlaka za serikali za Mitaa za serikali ya mapinduzi Zanzibar(Agosti 2018-Julai 2021),mradi Wa kuwajengea uwezo watumishi wa wizara ya mamlaka za serikali za Mitaa Katika uandaaji mipango na bajeti inayozingatia mahitaji ya watoto (Agosti 2018-Julai 2021)”, ameeleza Prof. Mayaya.

Hata hivyo amesema miongoni mwa  miradi ni pamoja na mradi wa kuandaa mipango mikakati Tanzania Bara (Julai 2020-2021)na mradi wa tathmini ya mbinu za upangaji wa mipango ya maendeleo na uhusishaji wa programu ya O&OD Katika mitaala ya vyuo vyuo vya elimu ya juu (2020-2021).

MWISHOO



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.