Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

WAZIRI BASHUNGWA, TOZO ZIMEKUWA MWAROBAINI UJENZI WA VITUO VYA AFYA,ELIMUMSINGI NA MIUNDOMBINU NCHINI

Imewekwa tar.: September 1st, 2022

OR - TAMISEM, DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilitoa Shilingi bilioni 117 za Tozo za Miamala ya Simu kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 234 kwenye Tarafa na Kata ambazo hazikuwa na Vituo vya Afya.

Bashungwa ameyasema hayo Jijini Dodoma leo tarehe 01 Septemba, 2022 katika mkutano na vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala ya tozo kwenye miamala ya Simu na benki ulioandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango.

Amesema kuwa ujenzi wa kila Kituo cha Afya umegharimu Shilingi milioni 500 na umefanyika kwa upelekaji wa fedha kwa awamu 2, ambapo awamu ya kwanza zilipelekwa Shiilingi milioni 250 na baadae Shilingi milioni 250 kukamilisha.

”Haijapata kutokea tangu tupate uhuru, kujengwa Vituo 234 kwa wakati mmoja ndani ya mwaka mmoja wa fedha ambapo ujenzi ulihusisha majengo ya Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara, Jengo la Wodi ya Wazazi, Jengo la Upasuaji na Jengo kwa ajili ya Kufulia” amesema Bashungwa.

Ameendelea kufafanua kuwa Serikali imejenga miundombinu sambamba na ununuzi wa vifaa vya kisasa ambapo jumla ya shilingi bilioni 145.5 kwa  ajili ya ununuzi wa vifaa tiba katika vituo hivyo 234 kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Pia amesema Serikali imeajiri watumishi wa Sekta ya afya 7612 kwa ajili ya kwenda kutoa huduma katika vituo hivyo vya kutolea huduma bora kwa wananchi.

Aidha, Bashungwa amesema katika sekta ya elimu, jumla ya Shilingi bilion 7 zimetolewa kusaidia ukamilishaji wa maboma 560 ili kupunguza mlundikano wa wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa.

“Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa umahiri wake wa kuwajali wananchi wa Tanzania na kuwezesha miradi mikubwa kama hii” amesema.

Bashungwa amesema kuwa kwa upande wa elimu bila ada  Serikali imehakikisha sera ya elimu bila ada  katika mwaka wa fedha 2022/23 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 346.5.  

Vile vile, Waziri Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi ambayo ilipokea fedha mwishoni mwa mwaka wa fedha 2021/22 na ikamilike kwa wakati ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi ndani ya miezi minne baada ya kupokea fedha za ujenzi.




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.