Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Wauguzi wapongezwa, watakiwa kujipnaga kutoa huduma bora zaidi

Imewekwa tar.: May 18th, 2019


Serikali imewapongeza wauguzi wote nchini na kuwataka kutoa huduma bora zaidi na kuhakikisha wanaleta mabadiliko makubwa ya ubora wa huduma za afya na kumaliza kabisa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wateja huduma hususani kutokana na watumishi wachache wenye kauli zisizofariji.

Agizo hilo limetolewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba leo na Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Kiwilaya katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba iliyopo  Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida.

Amesema wauguzi nchini ni jeshi kubwa katika sekta ya afya kwa kuwa ndiyo wengi zaidi ukilinganisha na kada zingine hivyo, mnauwezo wa kuleta mabadiliko makubwa kwenye utoaji wa huduma bora kwa jamii iwapo wataamua kutumia taaluma zao kikamilifu.

Amesema wauguzi wakijitoa kwa wagonjwa na kuwahudumia kwa huruma na kuwajali kutasaidia kupunguza kero za afya nchini  na ubora wa huduma za kiuguzi ni muhimu katika kuwavutia watumiaji wa huduma kwani nyie ndiyo hukaa muda mwingi zaidi mteja.

 “kama ambavyo mmesema kwenye risala yenu kuwa, wauguzi wengi wanajitahidi kushika maadili ya fani ya uuguzi bali wachache wanatia dosari, nawaasa kutokukata tamaa na kutokuvunjika moyo bali waibueni wanaoharibu na wakataeni wasiojirekebisha msiwabembeleze kwa kuwa  , ni gharama kubwa kwa taifa kupoteza mteja mmoja sababu ya wauguzi wasio na maadili” Anasisitiza Dkt. Gwajima

Dkt. Gwajima amesema, kutokana na watumishi wachache wasiozingatia maadili ya taaluma za utumishi sekta ya afya wakiwemo matabibu, wauguzi na kada zingine zote, wateja wengi wanakuwa wanasita kuja vituoni kupata huduma na badala yake wanaishia kununua dawa na kunywa bila ushauri wa daktari ama wanaenda kutafuta huduma mbali zaidi kwa gharama kubwa zaidi na matokeo yake, wananchi wanakuwa wazito kujiunga na mifuko ya bima za afya.

Dkt. Gwajima amesema tabia ya baadhi ya watoa huduma kukatisha tamaa wateja haikubaliki hivyo kila kituo kiwe na mifumo hai ya kupata maoni ya wateja ili kutoa fursa ya wasio na maadili kuibuliwa na jamii.

Ameendelea kueleza kuwa, wauguzi wanauwezo wa kufanya mageuzi katika Sekta ya afya  kwa kutoa huduma bora zaidi kwa jamii, kuacha lugha zisizofariji kwani huduma ya kwanza katika kituo cha afya ni lugha inayotumika na kauli ni kipimo cha wito wa utumishi.

Amesema kuwa, iwapo huduma zitatolewa kwa ubora unaostahili na raslimali zote kusimamiwa vizuri, wananchi wengi watajiunga na bima ya afya hivyo, itapunguza utegemezi wa vituo kwa serikali kuu katika kumudu gharama za uendeshaji huduma kila siku. Aidha, serikali itabaki inawezesha mambo makubwa yanayohusu miundombinu na ajira.

“haiwezekani tushindwe kutumia fursa ya bima ya afya katika kuboresha huduma kwa sababu tu, wapo baadhi wanakatisha tamaa kwa kukosa maadili. Aidha, haiwezekani wananchi  wajiunge na bima ya afya halafu washindwe kutumia huduma na fedha hizo zisirudi serikalini, lazima tujipange kwa huduma bora kuanzia kauli, uwepo wa vipimo, dawa na mazingira bora kwa ujumla”

Akielezea kuhusu kujitathmini katika utendaji kazi wa watoa Huduma za Afya Nchini Dkt. Gwajima amewataka wauguzi na watumishi wote wa sekta ya afya  kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utendaji kazi kwa takwimu ili, kubaini uwingi wa kazi kwa kila mtumishi badala ya kutoa taarifa za ujumla jumla kuhusu upungufu wa watumishi.

“imeibuka tabia kila taarifa inayotolewa inataja upungufu wa watumishi lakini hakuna takwimu za uwingi wa kazi kwa watumishi waliopo sasa na unakuta baadhi ya vituo saa sita mchana wateja wameisha na ukichunguza zaidi utakuta hata baadhi ya watumishi waliopangwa zamu wengine hawakufika lakini ukiomba taarifa unaambiwa upungufu wa watumishi, je huwa tunachanganua kuwa hao waliopo huwa wamehudumia wateja wangapi tangu walipoingia kazini hadi wanatoka?”Amesema Dkt.Gwajima

Aidha amevitaka Vituo vya kutolea huduma kuwa, sambamba na kuboresha huduma wahakikishe wanaendelea kuwahamasisha wananchi kukata Bima ya afya ili kuondokana na utegemezi  kwa Serikali.

Wakati huohuo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Dkt. Hussein Sekopo amesema katika mwaka wa fedha 2018/2019 jumla ya Kaya 9231 zimejiunga na Mfuko wa afya ya Jamii kati ya Kaya 15,000/= zilizotarajiwa sawa na asilimi 61.5 na jumla ya fedha zilizokusanywa ni zaidi ya shilingi milioni 92.

Naye Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Iramba Bi. NocklaVicent amewashukuru wauguzi wote kwa kufanyakazi kwa ushirikiano, upendo na weledi jambo ambalo limefanya sekta ya afya  kuendelea kuimarika

Aidha wameishukuru Serikali kwa kuajiri watumishi wapya wakiwemo wa Sekta ya Afya Nchini jambo ambalo limesaidia kupunguza uhaba wa watumishi  na kuboresha huduma kwa wananchi

Na Angela Msimbira SINGIDA


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.