Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Watendaji msikae ofisini mkamilishe madarasa – Dkt. Dugange

Imewekwa tar.: December 21st, 2021

Na Fred Kibano, Mara

Serikali imewataka watendaji mkoani Mara kuhamia maeneo ambayo miradi ya ujenzi wa miundominu ya elimu inajengwa ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kabla ya tarehe 30 Desemba, 2021.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Dkt. Festo Dugange Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati akifanya kikao cha pamoja na Sekretarieti ya Mkoa wa Mara na baadhi ya watendaji wa Manispaa ya Musoma katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa uliopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara mapema hivi leo.

“sisi kama Watendaji, tunayo kazi kubwa sana ya kusimamia hii miradi kupitia fedha hizi ambazo Serikali imezileta lakini kuhakikisha miradi yote na shughuli zote zinatekelezwa ipasavyo, kama miradi kukamilika kwa wakati, inayo ubora lakini pia inaendana na thamani ya fedha kulingana na miradi husika”  

Dkt. Dugange amesema lengo la Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwenye miradi ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari yapatayo 12,000 na yale ya shule shikizi za msingi yapatayo 3,000 nchini yanatakiwa yawe yamekamilika kwa asilimia 100 ifikapo Desemba 30, 2021 ili wanafunzi waweze kusoma bila kusubiria awamu za kwanza au ya pili kwa shule za sekondari kwani Serikali imefuta machaguo yanayofuata.

Amesema mkoa wa Mara umefikia asilimia 68 ya ujenzi wa madarasa na hivyo watendaji wanatakiwa kushinda maeneo ya kazi ili kusimamia kazi zinazofanyika ili zimalizike kwa wakati na kwa ubora na thamani halisi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bw. Albert Msovela amesema mkoa wa Mara ulipangiwa kujenga madarasa 708 kati ya hayo 618 ni ya shule za sekondari na madarasa 90 ni ya shule za msingi kwenye vituo shikizi.

Aidha, Bwana Msovela amesema mkoa ulipokea kiasi cha shilingi Bilioni 15 na milioni 780 kutekeleza ujenzi huo na mpaka sasa wamefikia asilimia 68 ya ujenzi wote kimkoa kutokana na changamoto mbalimbali kwa baadhi ya halmashauri kupata changamoto kadhaa lakini wamejipanga kukamilisha ujenzi huo katika muda uliowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kukabidhi mradi Serikalini.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Halfan Haule amesema changamoto kadhaa zilizojitokeza kwa Halmashauri kama upatikanaji wa saruji, vifaa kama mabati na bei ya bidhaa nyingine za ujenzi ambazo zimesababisha kuchelewa kwa miradi ya elimu lakini wamejipanga kukabidhi miradi hiyo tarehe 30 Desemba, 2021 kama iliyopangwa na Serikali.





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.