• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Watanzania waishio Marekani wachangia vifaa tiba vya thamani ya sh.milioni 15

Imewekwa tar.: April 21st, 2021

Na Atley Kuni, TAMISEMI

Watanzania waishio nchini Marekani wametoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 15 kwa mikoa 11 ya Tanzania bara, ikiwa ni mchango wao katika kutathamini juhudi za serikali katika kuimarisha afya za watanzania.

Vifaa hivyo vitagawiwa katika Mikoa ya Dar-es Salaam, Dodoma, Kigoma, Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Ruvuma, Mbeya, Lindi na Njombe.

Akipokea msaada huo wa vifaa tiba ambavyo vinatumika kupima kiasi cha Oxygen  mwilini  mwa mwanadamu, Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya, Dkt. Festo Dugange amewapongeza watanzania hao kwa kuthamini juhudi za serikali za kujenga na kukarabati miundombinu mbalimbali ya afya nchini.

 Ili kuhakikisha kuwa jukumu hilo linatekelezwa kikamilifu, Naibu Waziri ameongeza kuwa katika bajeti ya mwaka 2021/22 serikali imetenga shilingi bilioni 12.3 kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba.

“Serikali imefanya kazi kubwa ya ujenzi wa Miundombinu na katika mwaka wa fedha 2021/22 tumeweka kwenye bajeti ya dawa na vifaa tiba kama hivi na vingine kiasi kinachofikia Bil.12.3, hivyo kwa jitihada hizi za wadau hawa na wengine wote watakao kuja hapo baadaye ni ishara kwamba lengo letu la kuweka vitendanishi na dawa litatimia,” amesema Dkt. Dugange.

Akiongea kwa niaba ya watanzania waishio nchini Marekani, rais wa chama hicho, Dkt. Frank Minja, amesema, wanaona fahari ya kuchangia vifaa hivyo ambavyo vitakwenda kugawiwa kwenye ngazi ya Hospitali za Wilaya na kutumika na watanzania wenzao.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe. Neema Lugangira, ambaye amekuwa akishikirikiana na wadau hao, amesema hizo ni hatua za awali za kuwashirikisha watanzania mbalimbali kusaidia sekta ya afya lakini shabaha yake ni kuhakikisha kuwa wadau wengi zaidi wanapatikana kuchangia juhudi hizo.

“Sisi tunamshukuru sana Waziri wa Nchi Mhe. Ummy Mwalimu, kuridhia kupokelewa kwa msaada huu, ambao umepokelewa na Naibu Waziri, Dkt. Festo Dugange, mimi kama mbunge nitaendeleza jitihada hizi kwa niaba ya Serikali ili lengo la kuimarisha afya ya mtanzania iweze kutimia,” amesema Lugangira.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe, amesema kuwa atahakikisha kuwa vifaa vilivyopokelewa vinatunzwa ili viweze kudumu kwa muda mrefu.

Hafla ya kukabidhi vifaa tiba ilifanyika makao makuu ya Ofisi ya Rais TAMISEMI jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na Mkurugenzi wa huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe  na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utumishi wa Walimu Paulina Mkwama.

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.