• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Wakuu wa Mikoa watakiwa kuongeza kasi katika kusimamia ukusanyaji mapato

Imewekwa tar.: March 16th, 2021

Na Atley Kuni, DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha, wanaongeza kasi katika kuwasimamia watendaji walio chini yao ili waweze kukusanya mapato ya kutosha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuongeza uwezo wa kutoa huduma za jamii katika maeneo yao.

Akifunga kikao kilicho wakutanisha Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa yote 26 ya Tanzania bara leo jijini Dodoma kuhusu mapitio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22, Waziri Jafo amesema ukusanyaji wa mapato ya kutosha kutasaidia kuondokana na changamoto ya ufinyu wa ukomo wa bajeti (ceiling) katika mipango na bajeti za mikoa yao.

Amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanawahimiza watendaji wao kutumia mashine za kielektroniki katika kukusanya mapato  na wahakikishe kuwa wanakuwa wadilifu  katika kusimamia mashine hizo.

“Hakikisheni matumizi za Mashine za kieletroniki za kukusanya mapato ya Halmashuri, sambamba na kuongeza mashine zingine, lakini pia mfanye usuluhishi wa kibenki ifikapo tarehe 10 ya kila mwezi,” amesema Mhe. Jafo  

Mambo mengine aliyo yasisitiza Waziri huyo ni pamoja na usimamizi wa miradi na matumizi ya fedha za serikali ili tija iliyokusudiwa iweze kuonekana, Usimamizi wa Ugawaji wa Vitambulisho vya Wafanyabiashara Wadogo na Watoa Huduma Wadogo ambapo hadi sasa vitambulisho milioni 1.6 vimetayarishwa tayari kwa ajili kundi hilo la wafanya biashara, watakaofanya maombi kwa njia ya mtandao.

Pia amewataka viongozi hao kusimamia ukusanyaji wa kodi za majengo na ushuru wa mabango katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Usimamizi wa Elimumsingi bila Malipo na kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anaandikishwa kuanza masomo.

Jafo amewataka vilevile viongozi hao, kusimamia ukarabati na ujenzi wa vituo vya Afya kwani Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya ili kutokomeza maradhi na pia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito ili jamii iwe na afya njema na ishiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi.

“Mnapaswa kuhakikisha kuwa, wananchi wanapata huduma za ugani za kilimo, mifugo na uvuvi kwa urahisi, lakini pia kudhibiti ubora wa pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na mamlaka za utafiti na udhibiti, ujenzi wa miundombinu ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na kuboresha ushirika na masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi,” amesisitiza.

Agizo lingine kwa Viongozi hao ni kuwataka kufanya maandalizi ya Uwasilishaji wa Bajeti za Mikoa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwani ni takwa la Kikanuni kwa kila Mkoa kuwasilisha bajeti yake katika Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ambayo itaanza kupitia bajeti za Mikoa tarehe 18 Machi, 2021 hadi tarehe 26 Machi, 2021, ambayo ndiyo itakuwa siku ya Majumuisho.

“Hakikisheni mnafanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taarifa zinazowasilishwa zinajitosheleza na pia zimezingatia maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Kamati,” amesisitiza.

Awali akitoa mwelekeo wa Bajeti Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema lengo la kikao hicho ni kujadili sura ya bajeti na mwelekeo wake, lakini pia kupokea maoni ya viongozi hao kwa ajili ya maboresho kabla yakuwasilisha hatua inayofuata kwenye kamati za Bunge.

Akishukuru kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala, Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa, Mhandisi, Evaristi Ndikilo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, aliahidi kwenda kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa, kwani shughuli wanayo ifanya ni ya wananchi na wao wamepewa dhamana ya kuwahudumia wananchi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo.

MWISHO


Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.