• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wapewa wiki mbili kuboresha magodoro ya hospitali

Imewekwa tar.: May 26th, 2019

Na Mathew Kwembe, Dar es Salaam

Serikali imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na wa Halmashauri kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuanzia sasa wawe wamekwishanunua vitambaa vigumu vya mpira ambavyo hutumika kuyafunika magodoro yanayotumiwa na wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili yasiweze kuharibika kwa haraka.

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima wakati alipofanya ziara kutembelea  hospitali ya Vijibweni iliyopo eneo la Kigamboni  jijini Dar es salaam.

Amesema anatoa siku 14 kuanzia sasa kwa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri kuhakikisha kuwa magodoro yaliyopo kwenye Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwenye mikoa yao yanashonwa na kuwekea mifuko maalum ya mpira ili kuyafanya yarudi katika ubora wake.

Ameongeza kuwa kumekuwa na mtindo kwa baadhi ya watendaji wa halmashauri  kusingizia uchakavu wa magodoro na vitanda kwa vile tu Bohari kuu ya Dawa ilileta magodoro yenye vitambaa laini vya mpira na ni siku nyingi tangu  magodoro hayo yaletwe.

“Watendaji wengine wamekuwa wakidai kuwa MSD wametuuzia magodoro haya siku nyingi na kitambaa chake laini hivyo yameanza kuchoka,”amesema na kuongeza:

“Wakati inawezekana kununua kitambaa cha mpira, kwenye maduka yaliyopo yanayouza vitambaa vya mpira, mafundi wapo na kwa kuwatumia mafundi wenyeji wakashona magodoro haya yakarudi kuwa  mapya,” amesema.

Dkt Gwajima ameongeza kuwa hakuna sababu kwa watendaji hao kutumia visingizio vyao kwani bei ya kununulia mita kadhaa za vitambaa vigumu vya mpira  na za mashono ni ndogo na ni gharama zilizo ndani ya uwezo wa vituo vyetu vya kutolea huduma za afya.

Wakati huo huo, Dkt Gwajima amesifu hatua ya uongozi wa hospitali ya Vijibweni iliyopo wilayani Kigamboni kwa kuamua kukopa mashine ya Xray kutoka MSD ili waweze kuwahudumia wananchi walio wengi.

Amesema hatua hiyo ni nzuri kwani itawaondolea kero wananchi wengi waliokuwa wanalazimika kufuata huduma hiyo mbali na eneo hilo hivyo Dkt Gwajima amezitaka halmashauri nyingine za wilaya nchini kuiga mfano wa hospitali hiyo kwa kuhakikisha kuwa wanatumia vyanzo vyao vya mapato ya ndani kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

“Tunazo hospitali zetu nyingi ambazo zinasubiri mgao wa serikali, hii haiwezekani, tunachosema ni kwamba kila hospitali itasimama yenyewe kupitia timu yake ya usimamizi huduma za afya ya halmashauri kwa kupanua wigo wa huduma  na kuvutia wateja wengi zaidi kutumia huduma hizo badala ya kuzifuata mbali na makazi yao kwa gharama kubwa,” amesisitiza Dkt Gwajima.

Naibu katibu Mkuu ameongeza kuwa kupitia uchangiaji wa huduma hizo kama walivyofanya Vijibweni ni dhahiri kuwa, vituo husika vitaweza kumudu gharama za kununua mahitaji mbalimbali ya kuboresha huduma za afya badala ya kutegemea serikali tu.

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa misongamano ya  wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, Dkt Gwajima amesema pamoja na ukweli kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na upungufu wa watumishi, yapo baadhi ya maeneo ambayo upungufu huo unachangiwa na uzembe wa baadhi ya watoa huduma katika kuwajibika.

“Baadhi ya wataalam huwa wanachelewa kufika kazini na wakifika wanaishia kuona idadi ndogo ya wateja chini ya kiwango cha walau wateja 30 hadi 40 kwa siku kilichopo kwenye miongozo,” amesisitiza Dkt Gwajima

Aidha, amesema kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo yana watoa huduma wengi zaidi kuliko ilivyotakiwa nayo haya yanahitaji kupanguliwa wapelekwe waliko wachache.

Dkt Gwajima ameeleza kuwa ni kweli upungufu upo ila, upungufu huo hauwezi tu kupimwa kwa maneno ya mazoea bali kwa kupima uwingi wa kazi kwa kila mtoa huduma kwa wakati huo.

“Kupitia utaratibu wa kupima uwingi wa kazi kwa wakati wa sasa (workload) inawezekana kuchochea uwajibikaji wa mtumishi mmoja mmoja na kuleta uwiano sawa wa kazi miongoni mwa watumishi wa vituo mbalimbali na siyo baadhi wanasema kuna upungufu wa watumishi akiulizwa amehudumia wateja wangapi unakuta hata kumi hawafiki,” amesema.

Dkt. Gwajima amesema, lazima hoja ipimwe kwa takwimu ndipo tutaweza kujiridhisha kwani maeneo yote hayafanani.

Pamoja na kutembelea hospitali ya Vijibweni, Dkt Gwajima alipata fursa pia ya kutembelea na kushuhudia ujenzi wa hospitali za wilaya za kigamboni na Ilala ambapo kwa upande wa hospitali ya Kigamboni Naibu Katibu Mkuu aliusifu uongozi wa halmashauri hiyo kwa usimamizi thabiti uliopelekea majengo ya hospitali kuwa katika hatua ya kupaua tofauti na wenzao wa Manispaa ya Ilala ambao wao majengo matatu kati ya saba yapo katika hatua za msingi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Yudas Ndungile amesema kuwa wao wameyapokea maagizo ya Naibu Katibu Mkuu na kwamba maagizo hayo yanatekelezeka kwa vile yapo ndani ya uwezo wa mkoa wake.

Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea mikoa ya Dar es salaam na Pwani ambapo kabla ya hapo alitembelea mikoa ya Morogoro, Dodoma, Njombe, Ruvuma, Iringa na Manyara.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Fomu za kujiunga na Kidato cha kwanza 2024 December 16, 2024
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA UNUNUZI WA MAGARI YA WAGONJWA.

    May 12, 2025
  • Mhandisi Mativila aridhishwa Utekelezaji wa Miradi ya Barabara ya Mtili-Ifwagi na Sawala-Iyegeya

    May 11, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.