Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Vyuo vya Serikali vyatakiwa Kujiendesha Kibiashara

Imewekwa tar.: December 8th, 2023

Na Fred Kibano, Dodoma

Serikali imevitaka vyuo vyote nchini kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea ruzuku ya fedha za matumizi yao kutoka Serikali Kuu.

Akihutubia katika mahafali ya 15 tarehe 07 Novemba, 2023 Hombolo nje kidogo ya Jiji la Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Deogratius Ndejembi ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amevitaka vyuo vyote nchini kujiendesha kibiashara kwa kubuni vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na kuwatatumia Watafiti wabobezi kufanya tafiti.

“Chuo hiki kinayo hazina ya Wabobezi wa fani mbalimbali fanyeni utafiti na kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kupunguza utegemezi, vilevile endeleeni kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo na shughuli nyingine zinazohusu ustawi wa chuo” alisema Mhe. Ndejembi.

Mhe. Ndejembi pia alisema azma ya Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alifanya kikao na Watendaji wa Taasisi mbalimbali nchini mwezi Agosti, 2023 ni kuona mashirika ya Umma yanaongeza tija katika uzalishaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Mfuko wa Serikali Kuu.

“nasisitiza mashirika na Taasisi za Serikali ziendelee kubuni mikakati ya kuongeza mapato ili faida itumike kuendesha shughuli za Taasisi na kutoa gawio Serikalini, maelekezo haya yanahusu pia jumuiya ya chuo hiki, ongezeni kasi ya kuibua mikakati inayotekelezeka na yenye tija” alisema Ndejembi.

Mheshimiwa Ndejembi akijibu kuhusu kero ya kuwekwa lami barabara ya Ihumwa hadi Hombolo alisema tayari upembuzi yakinifu umefanyika lakini ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kazi ianze kwa wakati baada ya kukamilika taratibu zote.

Akisoma risala kabla ya hotuba ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) Prof. Joseph Kusilwa alitoa ombi la kupatiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo pacha ya kampasi ndani ya jiji la Dodoma baada ya kupata eneo la ilipokuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ili kuondokana na adha ya kulipa kodi inayofikia shilingi milioni 75 kwa mwaka kwani upembuzi yakinifu umekwishafanyika lakini ufinyu wa bajeti ni kikwazo kwao. 

Kwa upande wake akitoa maelezo ya awali, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) Dkt. Mashala Yusuph alisema chuo hicho kimepewa jukumu la kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, kufanya tafiti na kutoa ushauri elekezi ambapo mpaka sasa fani sita zinatolewa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja ambao ni Mamlaka za Serikali za Mitaa. 

Aidha, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Chuo cha Utumishi wa Umma, Chuo kimetoa mafunzo mbalimbali mwaka huu yakiwemo mafunzo kwa Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa kwenye mikoa 12. 

Naye Mlau wa chuo hicho Dkt. Danford Sanga amesema jumla ya wahitimu 4,666 wamehitimu katika mahafali hayo ya 15 tangu chuo hicho kianze kutoa mafunzo ya muda mrefu mwaka 2007 kwa ngazi za astashahada ya awali, stashahada na shahada ya kwanza na kwamba matarajio yao ni kuona wahitimu hao wanatoa huduma bora kwa jamii zinazowazunguka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya wananfunzi Stephen Thomas alitoa ombi la kupatiwa mikopo kama ilivyo kwa vyuo vingine vya kati ili waweze kujikimu katika masomo yao, pia kupatiwa kipaumbele kwenye ajira za Serikali na kuwekwa lami kwa barabara ya Ihumwa hadi Hombolo ili kuondoa adha ya usafiri na kukipa chuo hicho hadhi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha  huduma ya afya ya msingi.

    May 24, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.