Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Vishikwambi vitumike kuhamasisha matumizi ya TEHAMA – Waziri Mkuu Majaliwa

Imewekwa tar.: November 5th, 2022

Na Fred Kibano – OR TAMISEMI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi kwa walimu wa ngazi zote ili kuboresha utoaji wa elimu kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 4.11.2022 katika Ukumbi wa jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali Mtumba nje kidogo ya Jiji la Dodoma wakati akitoa hotuba yake na kugawa vishikwambi kwa walimu wa ngazi zote wakimwemo wakufunzi wa vyuo na kuagiza kwamba ni lazima vitumike kama azma ya Serikali ilivyokusudia ya kuhamasisha na kuboresha TEHAMA katika Ufundishaji na Ujifunzaji nchini.

“kumekuwa na uhitaji wa vifaa vya TEHAMA katika shule zetu hasa walimu wetu katika maandalizi hayo ya ufundishaji na Ujifunzaji pamoja na usimamizi, upimaji na tathmini katika Sekta ya elimu nchini” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesema lengo la kuzindua ugawaji wa vishikwambi kwa walimu wote nchini ni kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kupitia TEHAMA lakini hatapenda kuona vishikwambi hivyo vinakwenda kwa watu wasio walengwa.

“kwa msingi huo naelekeza kwamba wahusika katika ugawaji hakikisheni vishikwambi hivi vinawafikia walengwa waliokusudiwa” amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa ameziagiza Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya habari kutoa mafunzo ya matumizi ya vishikwambi kwa walimu na kwamba vitakuwa ni mali ya mwalimu mwenyewe lakini pia hatapenda kuona vinazagaa mitaani.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imekusudia kujenga chuo cha kisasa cha TEHAMA eneo la Nala Jijini Dodoma ili kuongeza kasi,na ubunifu katika matumizi ya TEHAMA lengo likiwa ni kusaidia vijana kuendeleza ubunifu wao na kuonyesha namna ambavyo wanaweza kuunda vifaa mbalimbali.

Akitoa neno kabla ya hotuba ya Mgeni rasmi, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema jumla ya vishikwambi 300,000 vilinunuliwa na Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambapo baadhi vilitumiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), vishikwambi 6,600 vilitumika upande wa Zanzibar na vishikwambi 293,400 Tanzania Bara ambapo vilivyotumika Tanzania Bara vinagawiwa kwa walimu wa ngazi mbalimbali.

Prof Mkenda ameyataja makundi hayo kuwa ni pamoja na walimu wa shule za msingi za Serikali (185,404), walimu wa sekondari za umma (89,805), Wathibiti Ubora wa Wilaya na Kanda (1,666), Wakufunzi wa vyuo vya Ualimu (1,353), Wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii (297), Wakufunzi wa vyuo vya Ufundi Stadi (996), Maafisa Elimu Mkoa, Wilaya na Kata (5,772) na Baraza la Mitihani (8,357).  


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.