Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Uongozi Jiji la Dodoma wapewa wiki moja kukamilisha kibali cha ujenzi

Imewekwa tar.: October 30th, 2018


Na Mathew Kwembe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa ametoa kibali cha ujenzi wa uzio wa shule ya Sekondari ya Dodoma ndani ya wiki moja kuanzia leo.

Agizo hilo amelitoa leo wakati wa Mahafali ya Kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Dodoma ambapo jumla ya wahitimu 223 walikabidhiwa vyeti vyao vya kumaliza kidato cha nne na Waziri wan chi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dodoma Mwalimu Amani Mfaume, ni zaidi ya mwaka sasa uongozi wa shule hiyo umekuwa ukihangaikia kibali hicho bila mafanikio yoyote.

Kufuatia maelezo hayo, Waziri Jafo alimwagiza Mkurugenzi wa Jiji kuhakikisha kuwa ifikapo jumanne ijayo kibali hicho kiwe kimepatikana na kuahidi kuitembelea shule hiyo siku hiyo ili kujionea utekelezaji wa agizo lake hilo.

Kadhalika Waziri Jafo aliuagiza uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa linaratibu zoezi la uchangiaji fedha kwa wadau mbalimbali wa jiji la Dodoma hususani wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Dodoma ili zipatikane fedha za ujenzi wa uzio huo.

Mhe.Jafo alilitaka jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa zoezi la ujenzi wa uzio huo uwe umekamilika ifikapo januari 2019, ili wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waondokane na bughudha wanayoipata sasa ambapo kutokana na kutokuwepo uzio, kumekuwa na vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na wapita njia.

Alisema kutokana na shule hiyo ya sekondari kuwa katikati ya Jiji la Dodoma wanafunzi wa shule hiyo hasa wasichana ambao wanaishi katika mabweni yaliyopo ndani ya shule hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali kutoka kwa raia wasio wema waishio jijini Dodoma.

Wakati huo huo Waziri Jafo   amelitaka jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa inaisimamia vyema shule ya sekondari ya Dodoma ili iweze kupata matokeo mazuri katika mitihani ya kidato cha nne inayotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Alisema kuwa haiwezekani shule hiyo yenye walimu 70 kutoa wanafunzi watano tu ndiyo waliopata daraja la kwanza mwaka jana, na hivyo akaagiza uongozi wa jiji kuliangalia suala hilo kwani ni aibu kwa shule hiyo wanafunzi wake wengi kupata daraja sifuri.

Aliongeza kuwa kama alivyofanya katika wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha kampeni ya tokomeza ziro, anatarajia kuwa Jiji la Dodoma litafanya hivyo kwa kuanzia na shule hiyo ya Sekondari Dodoma kuhakikisha kuwa inapunguza idadi ya wanafunzi wanaopata daraja sifuri kutoka 60 na 70 ilivyo sasa kwa mwaka hadi wanafunzi chini ya watano.

Aliahidi kuwa endapo shule ya Dodoma itafaulisha zaidi ya wanafunzi 20 katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne na wanafunzi pungufu ya watano watapata daraja sifuri, ataandaa sherehe kubwa kuwapongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.