Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Shirika la UNFPA lapongezwa kwa ujenzi wa jengo la upasuaji Kituo cha Afya Nassa

Imewekwa tar.: February 28th, 2019

Na Mathew Kwembe, Simiyu

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani (UNFPA) limepongezwa kwa ujenzi wa jengo la upasuaji na wodi ya mama na motto katika kituo cha Afya Nassa kilichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Pongezi hizo zilitolewa jana na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya hiyo  Dkt Godfrey Mbangali mbele ya Mratibu wa shirika la UNFPA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Dinah Atinda mara baada ya kutembelea majengo mapya ya upasuaji na wodi ya mama na motto katika kituo hicho.

Aliongeza kuwa kuwepo kwa majengo hayo kumesaidia sana katika kuboresha huduma katika eneo hilo na hivyo kuondokana na mtindo wa kuwa na wagonjwa waliokuwa wakirundikana sehemu moja na sasa  wamepata fursa ya  kupata huduma ya upasuaji.

Dkt Mbangali alisema kuwa kukamilika kwa majengo hayo kumewezesha kuanzishwa kwa huduma za upasuaji katika kituo hicho cha afya na hivyo kuwapunguzia adha ya kwenda kufuata huduma za upasuaji kwa wakazi wa wilaya hiyo wapatao 203,597 katika Hospitali teule ya Bariadi na Hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Aliongeza kuwa kabla ya kuanzishwa kwa huduma za upasuaji kituoni Nassa mgonjwa alilazimika kupewa rufaa kwenda Hospitali teule ya Bariadi na kisha alitakiwa kupelekwa Bugando mwanza kama angehitajika kupata rufaa zaidi.

“Ukiangalia jiografia ya jimbo la Busega ambalo linapakana na mkoa wa mwanza mgonjwa angelazimika kuzunguka kwanza kwenda Bariadi na kisha kupelekwa Bugando Mwanza, ambapo ni mzunguko mrefu,” alisema.

Kulingana na mazingira ya kijiografia ya wilaya ya Busega, kama kusingekuwa na huduma ya upasuaji, mgonjwa kwanza angelazimika kwenda Bariadi na kama angezidiwa zaidi angelazimika kupelekwa jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Dkt Mbangali aliongeza kuwa mbali na wilaya hiyo kuwa na vituo vya afya vinne lakini ni kituo cha Nassa pekee ndicho kinachotoa huduma za upasuaji wilayani humo.

Aliongeza kuwa tangu huduma za upasuaji  zianze kituoni hapo, jumla ya wagonjwa 12 wamekwishafanyiwa upasuaji  wilayani humo na wote wanaendelea vizuri baada ya kupata huduma hizo.

Mbali na ujenzi wa jengo, UNFPA pia walitoa vifaa mbalimbali vinavyohitajika maabara kama vile vitanda, mashine ya usingizi  pamoja na mashine ya kufyonza damu ili sehemu iliyofanyiwa huduma za upasuaji iweze kupona kwa haraka.

Naye Mratibu wa UNFPA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Dinah Atinda alisema kuwa kituo cha Nassa ni miongoni mwa vituo na zahanati 38 kutoka mkoa wa Simiyu ambazo zilipata fedha za ujenzi wa majengo ya wodi ya wazazi na jengo la upasuaji ambapo kituo hicho kilipokea jumla ya shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo ya mama na mtoto na  jengo la upasuaji na shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mingine katika kituo hicho ukiwemo ujenzi wa jengo la maabara.

Pia Bi Atinda aliusifu uongozi wa wilaya ya Busega kwa kuweza kusimamia kikamilifu fedha za serikali katika ujenzi wa majengo hayo mawili.

Mbali na Kituo cha Afya Nassa, UNFPA walifadhili ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati za Kiloleli, Badugu, Igalukilo, Ngasamo na Nyamikoma

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.