Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Ujenzi Hospitali za Wilaya Ukamilike kwa Wakati – Mhandisi Nyamhanga

Imewekwa tar.: February 17th, 2019

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka Watendaji wa afya katika Mikoa na Wilaya kusimamia matumizi ya fedha za Umma katika ngazi zote na kukamilisha miradi ya zahanati, hospitali za wilaya na vituo vya afya ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Mhandisi Nyamhanga ametoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake katika Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela na kukagua miradi ya maendeleo ambapo kwa upande wa afya alikagua ujenzi wa kituo cha afya Igoma cha Jijini Mwanza na kituo cha afya Karume na hospitali ya wilaya zote za Manispaa ya Ilemela.

“zingatieni matumizi ya fedha kwa kuwa na usimamizi makini katika ngazi zote na tumieni mashine za kielektroniki kukusanya mapato ya Serikali, jengani majengo kwa gharama nafuu yanayozingatia ubora unaotakiwa na kukamilisha ujenzi kwa wakati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi” alisema Mhandisi Nyamhanga

Aidha, Mhandisi Nyamhanga amesema mpaka hivi sasa katika sekta ya afya, Serikali imejenga jumla ya vituo vya afya 304 nchini kote na hospitali za wilaya 67 ambazo zinaendelea kujengwa na kila hospitali mpya ya wilaya imekwisha pelekewa kiasi cha fedha shilingi bilioni moja na nusu.

Nyamhanga ameagiza ujenzi wa hospitali mpya ya Manispaa ya Ilemela ijengwe kwa kufuata ubora na kukamilika kwa wakati ili kufikia kufikia juni, 2019 ujenzi huo uwe umekamilika kwa asilimia mia moja.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza Dkt. Juma Mfanga amesema kituo cha afya Igoma kimejengwa kwa kutumia nguvu za wananchi ambapo wamefanikiwa kujenga majengo sita ambayo ni jengo la upasuaji, jengo la wodi ya wazazi, jengo la maabara, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la mionzi (x – ray) na jengo la kufulia nguo za wagonjwa.

Dkt. Mfanga amesema kukamilika kwa majengo ya kituo hicho licha ya kukabiliwa na changamoto ya watumishi, tayari kimepunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, hospitali ya rufaa ya Sekou toure na hospitali ya rufaa ya kanda Bugando mkoani Mwanza.

                                             

                                                 anaandika Fred Kibano


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

    June 14, 2025
  • MANYARA NA MWANZA MABINGWA RIADHA MITA 800 

    June 14, 2025
  • HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU  KATIKA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO- ADOLF NDUNGURU 

    June 13, 2025
  • WAVU KWAENDELEA KUNOGA UMITASHUMTA

    June 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.