• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Ubungo Yazindua Rasmi Mikopo ya Wanwake na Vijana Yenye Thamani ya Tsh. Bil 1.9

Imewekwa tar.: May 3rd, 2018

Katika kuhakikisha wananchi wa Ubungo wanawezeshwa kiuchumi Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo leo imeweka historia ya kuzindua rasmi utoaji wa mikopo ya wanawake na vijana katika viwanja vya Barafu Mburahati Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Akizindua mikopo hiyo Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI *Mh.  Joseph Kakunda* kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI *Mh. Selemani Jafo* ameipongeza Halmashauri ya Manispaa Ubungo kwa kuwa mfano wa kuigwa licha ya uchanga wa Manispaa hiyo imeweza kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani nakufikisha kiasi cha Tsh *1.9 Bilioni* kwa ajili ya Wanawake na Vijana.

Na katika mchakato ujao ameuagiza Uongozi wa Manispaa kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya vikundi maalumu vya walemavu na wenyewe wapate mikopo hiyo waweze kujikwamua kiuchumi.

Sambamba na hilo Mh. Kakunda ameahidi kumwagiza Katibu Mkuu TAMISEMI kuandika barua ya pongezi kwa Manispaa ya Ubungo Kwa kuwa Manispaa ya mfano kwa kutenga kiasi kikubwa cha fadha licha ya kuwa ndio kwanza ina takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa.

Pia kuanzia bajeti ijayo ya mwaka wa fedha ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatenga sehemu ya Mapato yake ya ndani asilimia 10 kwa ajili ya wanawake na Vijana na itakuwa moja ya kigezo cha kupima utendaji kazi wa viongozi katika Halmashauri husika.

Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikabidhi hundi mbili za mfano kwa vikundi viwili. Kikundi cha kwanza ni kikundi cha vijana Mabu Group ambacho kilipokea hundi ya Tshs milioni saba kwa niaba ya vikundi vya vijana. Kikundi cha pili ni Energy Women Group ambacho kilipokea hundi ya Tshs milioni 18.2. Katika kiasi kilichotengwa, vikundi 365 vinatarajia kufaidika na mkopo huo.

Amesisitiza wanawake na vijana  wa Manispaa ya Ubungo kutumia fursa hiyo  kwa kuwa itawaongezea kipato na baadae kuwa na jamii yenye wanawake na Vijana wenye Ustawi.

Kwa upande wa Uongozi  wa Manispaa ya Ubungo Mh. Joseph Kakunda amewaagiza kuhakikisha wanatenga maeneo zaidi hata kwa kufidia ili vijana na wanawake wapate sehemu za kufanya biashara kwa amani.

Lakini pia amewataka CRDB kwa kuwa ndio weliopewa dhamana ya Kutoa mikopo hiyo, mikopo itolewe kwa utaratibu mzuri kusiwe na kero ya aina yoyote.

Naye mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg *John L. Kayombo* wakati akitoa taarifa ya mikopo hiyo amesema yeye kwa kila pesa inayoingia katika Manispaa kabla ya matumizi yeyote anatenga kabisa asilimia 10 kwa ajili ya Mikopo ya wanawake na vijana.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori alimshukuru Naibu Waziri kwa kuitikia wito wa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo. Aliongeza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya  Ubungo itaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa Halmashauri nyingine na itahakikisha inatenga asilimia 10 ya vijana na kinamama katika mapato yake ya kila mwaka wa fedha.

*Imetolewa na*

*Kitengo cha Habari na Uhusiano*

*Manispaa ya Ubungo*

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.