Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

TIMU YA WAWEZESHAJI YANOLEWA UTARATIBU MPYA MIKOPO YA ASILIMIA 10

Imewekwa tar.: July 9th, 2024

Na Fred Kibano, Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Adolf Ndunguru amefungua mafunzo ya mikopo ya asilimia 10 kwa wawezeshaji wa Kitaifa na kuwataka washiriki hao kuhakikisha wanaelewa vema ili kwenda kufundisha wengine kwa viwango vinavyokubalika.

Akifungua mafunzo hayo kuhusu utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa wawezeshaji wa Kitaifa mapema leo Julai, 9, 2024 jijini Dodoma, Ndunguru amewataka wawezeshaji hao kwenda kuwezesha mafunzo watakayoyapata ili malengo yake yaweze kutimia kwani Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza Mikopo irudishwe na isimamiwe kikamilifu.

“Ninafahamu kuwa uandaaji wa Kanuni, Mwongozo, vitini vya mafunzo pamoja na maboresho ya Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi umekamilika, niwapongeze wote mlioshiriki kukamilisha nyenzo zitakazowezesha utoaji wa mafunzo kwa wasimamizi na vikundi kabla ya  kuanza kutoa mikopo kama ilivyoelekezwa na Serikali,” alisema Katibu Mkuu Ndunguru.

Ndunguru amesema Serikali inatarajia kuona mafunzo hayo yanakwenda kutatua changamoto za utofauti wa uelewa na tafsiri ya baadhi ya vifungu vya kanuni kati ya Halmashauri moja na nyingine, kukosekana kwa utaratibu maalum wa utambuzi na uundaji wa vikundi vinavyotarajiwa kunufaika na mikopo ambapo ilisababisha kuwepo vikundi hewa, usimamizi usioridhisha wa mikopo inayotolewa pamoja na marejesho ambayo ilipekea kusababisha fedha nyingi za marejesho kutorejeshwa kwa wakati.

Pia amesema kukosekana kwa utaratibu mzuri wa usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli zinazofanywa na vikundi vilivyopewa mikopo, kukosekana kwa utaratibu mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za mikopo, marejesho, vikundi vilivyosajiliwa na shughuli zinazofanywa na vikundi na mapungufu ya Mfumo wa Kieletroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo.

Naye, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa wa Ofisi hiyo, Beatrice Kimoleta amesema baada ya Serikali kutangaza kurejesha mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imefanya masuala mbalimbali ikihusisha marekebisho ya  Sheria ya Fedha sura 29, mapitio ya Kanuni za Mikopo ya asilimia 10, uandaaji wa Miongozo na Vitini vya mafunzo.

Pia amesema baada ya mafunzo hayo jumla ya wawezeshaji 840 watajengewa uwezo na baada ya hapo watakwenda kutoa mafunzo kwa Kamati za Uratibu wa mikopo ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata kuhusu nafasi zao katika kusimamia utoaji wa mikopo ya vikundi.

Akitoa neno la shukrani Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Erick Kitali amemshukuru kwa mafunzo hayo na kuahidi kusimamia maelekezo yote ya Serikali yaliyotolewa kuhusu utoaji na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika ngazi zote.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamehudhuriwa na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wawezeshaji wa Mafunzo, Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.