Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Tatueni Changamoto za Walimu Kuleta Mabadiliko – Dkt. Msonde

Imewekwa tar.: April 5th, 2023

Na Fred Kibano - Mwanza

Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kuwasimamia walimu kwa weledi na kutatua changamoto zinazowakabili ili kuleta mabadiliko katika Sekta ya Elimu nchini.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo tarehe 04.04.2023 Jijini Mwanza na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (ELIMU) Dkt. Charles Msonde wakati akitoa maelekezo ya Serikali kwa Viongozi hao kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDEOA).

Dkt. Msonde amesema njia pekee ya kuleta mabadiliko kwenye Sekta ya Elimu ni uwajibikaji wa kuwasaidia walimu kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwenye mazingira yao ya kazi kama vile kuwa na kanuni ya ulipaji wa madeni ya walimu na kuyakabili masuala yote yanayohusiana na rushwa sehemu ya kazini.

“itakuwa ni kazi ngumu sana kwa walimu kuhubiri mabadiliko kama walimu hawa hatujawajali, changamoto za walimu ni nyingi na mazingira yao ya utendaji kazi yanahitaji sisi tuwasaidie zaidi” amesema Dkt. Msonde. 

Amesema kuwasimamia walimu katika ufundishaji unaozingatia watoto kupata ujuzi ambao utaleta matokeo makubwa kuliko ufundishaji wa kuzingatia kumaliza mada kwa wakati bila kuzingatia malengo ya Mkakati wa Ufundishaji na vigezo vyake 22 kama Kusoma, Kuandika na kuhesabu na umahiri katika somo la kiingereza kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

 Dkt. Msonde amewapongeza Viongozi hao kwa kuongeza kiwango cha uwajibikaji wa walimu nchini kutoka asilimia 30 iliyokuwepo hapo awali mpaka asilimia 60 iliyopo hivi sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Vicent Kayombo amesema kwa hivi sasa Viongozi hao wanafuatilia kwa karibu ufundishaji wa walimu shuleni lakini pia ili kuboresha Ufuatiliaji na Usimamizi wa elimu tayari magari yaliyoagizwa kwa ajili ya Seksheni ya Elimu ya Sekondari yameshawasili na yatapelekwa kwenye maeneo husika.

Kauli Mbiu ya Mkutano huo kwa mwaka 2023 wa REDEOA unasema ‘Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu Unaimarisha Ufundishaji, Ujifunzaji na Ustawi wa Walimu na Wanafunzi’


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NENDENI MKAITANGAZE SERIKALI.

    May 24, 2025
  • SOKO LA KISASA LA NYAMA CHOMA LAZINDULIWA VINGUNGUTI

    May 24, 2025
  • DKT. Biteko asisitiza wazazi kuthamini nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya mtoto.

    May 24, 2025
  • Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha  huduma ya afya ya msingi.

    May 24, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.